// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
TAIFA STARS YA BAADAYE YAENDELEZA DOZI, YAWATANDIKA ‘MAFUNDI’ WA TANGA 4-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINETAIFA STARS YA BAADAYE YAENDELEZA DOZI, YAWATANDIKA ‘MAFUNDI’ WA TANGA 4-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
TAIFA STARS YA BAADAYE YAENDELEZA DOZI, YAWATANDIKA ‘MAFUNDI’ WA TANGA 4-0
Na Mwandishi Wetu, TANGA TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15, U-15 leo imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu, baada ya kuichapa mabao 4-0 kombaini ya U-15 ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Ushindi huo umetokana na mabao mawili ya Issa Abdi dakika ya 21 na 23, Frank George dakika ya tisa na Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 80. Pamoja na ushindi huo, lakini vijana wa U-15 ya Taifa, walikutana na ushindani kutoka kwa wachezaji wenye vipaji wa U-15 ya Tanga. Kivutio zaidi alikuwa ni kiungo Joseph Yakobo ambaye Tanga wanamuita ‘Sure Boy’ na mshambuliaji George Chande aliyeisumbua mno ngome ya timu ya taifa iliyoongozwa na Nahodha, Maulid Lembe.
Wachezaji wa U-15 wakishangilia moja ya mabao leo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
Wachezaji wote waliokwenda majaribio Orlando Pirates ya Afrika Kusini mwezi uliopita, Asad Ali Juma, Issa Abdi Makamba, Kevin Deogratius Kahego, Amani Amede Maziku na Athumani Maulid Rajab walicheza leo. Huo unakuwa mchezo wa tano kushinda, kati ya mechi saba tangu kuundwa kwa timu hiyo Aprili mwaka huu, ikifunga jumla ya mabao 15 na kufungwa mawili tu. Timu hiyo iliifunga 4-1 na 3-0 Mbeya, ikaifunga 4-0 na 1-0 Zanzibar na kutoa sare ya 0-0 na 1-1 na Morogoro kabla ya ushindi wa leo. Timu hiyo inayoandaliwa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za vijana Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar zitakazoanza Juni mwakani, imekuwa ikiweka kambi kila mwishoni mwa mwezi kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu, chini ya kocha wake, Bakari Shime.
Kiungo wa U-15 ya taifa, Asad Ali juma akiwatoka wachezaji wa U-15 ya Tanga
Asad Ali Juma (kulia) akitafuta maarifa ya kumpokonya mpira mchezaji wa U-15 ya Tanga
Mshambuliaji wa U-15 ya Taifa, Amani Maziku akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa U-15 ya Tanga
Beki wa kushoto wa U-15 ya Taifa, Faraj John (kulia) akimtoka mchezaji wa Tanga
Kikosi cha U-15 ya Taifa kilichoifunga 4-0 Tanga leo
Kikosi cha U-15 ya Tanga kilichomenyana na U-15 ya taifa leo
Kesho, ‘Taifa Stars’ hiyo ya baadaye inatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho mjini hapa, itakapomenana na U-17 ya mkoa Tanga hapa hapa, Mkwakwani. Wachezaji wote wa timu hiyo ni wanafunzi wa sekondari mbalimbali nchini na ndiyo maana hukutanishwa mwishoni mwa mwezi tu kwa mazoezi ya pamoja.
Mostbet Türkiye Mobil Uygulamasını Indi
-
Mostbet Türkiye Mobil Uygulamasını Indir En İyi Bahis Empieza Online
Casino Platformu Content Mostbet’te Pasta” “oyunları Bir Kumarhane Için
Depozitoda ...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment