// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SUNDAY OLISEH ATUMIA 'MABAUNSA' KUMTIMUA ENYEAMA KAMBINI SUPER EAGLES - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SUNDAY OLISEH ATUMIA 'MABAUNSA' KUMTIMUA ENYEAMA KAMBINI SUPER EAGLES - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 07, 2015

    SUNDAY OLISEH ATUMIA 'MABAUNSA' KUMTIMUA ENYEAMA KAMBINI SUPER EAGLES

    Sunday Oliseh ametibuana na Enyeama
    KOCHA wa Nigeria, Sunday Oliseh amemfukuza kwenya kambi ya timu nchini Ubelgiji, kipa na Nahodha Vincent Enyeama baada ya kuchelewa kuingia kambini.
    Kipa huyo namba moja wa Lille ya Ufaransa, inaelezwa alibishana na kocha, kwa kuendelea kueleza sababu za kuchelewa kwake licha ya kuambiwa anyamaze na kuondoka.
    Na kipa huyo alipogoma kuondoka, kocha huyo aliwaita walinzi waje kumfukuza. Pamoja na Enyeama kutaka kujitetea, lakini hakupata fursa hiyo kwa Oliseh.
    Sakata hili linaibuka baada ya kipa huyo kurejea kambini akitoka kwenye mazishi ya mama yake.
    Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) limethibitisha mtafaruku baina ya wawili hao, lakini wakajaribu 'kupoza poza'. "Ni kweli kulikuwa kuna kutoelewana kidogo kambini, lakini tatizo hilo limetatuliwa na Enyeama amebaki kambini,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUNDAY OLISEH ATUMIA 'MABAUNSA' KUMTIMUA ENYEAMA KAMBINI SUPER EAGLES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top