// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAIS KIKWETE: WATU WANAPENDA ‘MISIFA’ YA KUITWA RAIS, MWENYEKITI LAKINI HAWASAIDII CHOCHOTE MICHEZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAIS KIKWETE: WATU WANAPENDA ‘MISIFA’ YA KUITWA RAIS, MWENYEKITI LAKINI HAWASAIDII CHOCHOTE MICHEZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 13, 2015

    RAIS KIKWETE: WATU WANAPENDA ‘MISIFA’ YA KUITWA RAIS, MWENYEKITI LAKINI HAWASAIDII CHOCHOTE MICHEZO

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kwamba siku hizi watu wanapenda umaarufu wa vyeo vya klabu na vyama vya michezo, lakini si kufanya kazi ndiyo maana michezo inadumaa nchini.
    Akizungumza katika hafla maalum ya kuagwa na wanamicheo, iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ukumbi wa Mlimani, City, Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema anashangaa kwa nini michezo nchi hii haiendelei.
    Rais Dk Jakaya Kikwete (katikati) wakati anaingia ukumbi wa Mlimani City jana. Kulia ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto na kushoto Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara

    Rais Kikwete alisema haoni sababu ya michezo kutoendelea nchini wakati kuna mazingira mazuri na katika kipindi cha miaka 10 ya utawala wake alijitolea mno kusaidia michezo.
    Alisema kubwa alilofanya ni kusaidia wataalamu kwa kuhakikisha kila mchezo unapata kocha naye ndiye anawalipa mishahara, lakini ajabu baadhi ya vyama vya michezo vilishindwa kundelea kufanya hivyo.
    “Netiboli walianza vizuri, walikwenda hadi Singapore kwenye mashindano ya dunia, lakini baadaye kilichowatokea sijui nini nini,”alisema.
    Rais Dk. Jakaya akasema vyama vinaweza hata kuajiri makocha wazawa na wakaendelea kulipwa kama walivyokuwa wanalipwa makocha wa kigeni.
    Akawageukia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambao wameamua kuachana na makocha wa kigeni na kuajiri mzalendo, Charles Boniface Mkwasa akiwaambia kwamba wahakikishe wanamlipa kama walivyokuwa wanalipa Wazungu.   
    Rais Kikwete amesema kwamba msaada wake wa mwisho ambao anawaachia wanamichezo wa Tanzania, ni kituo cha kulea vipaji vya wanamichezo wadogo cha Symbion Power kilichopo eneo la Kidongo Chekundu, Dar es Salaam ambacho kitazinduliwa Oktoba 17, mwaka huu. 
    Amesema kituo hicho kilichojengwa kwa msaada wa klabu ya Sunderland ya England kina vifaa na viwanja vya michezo aina yote, ukiwemo wa mpira wa kikapu wa kiwango cha viwanja vya Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA).
    Pamoja na hayo, Rais Kikwete aliwashukuru TASWA kwa kumuandalia shughuli hiyo na akasema atamshauri mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aendelee kuikumbatia michezo.
    Kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Mwameja Mohammed (kulia) na mpenzi wa Simba SC, Juma Ndabila
    Waandishi wa Habari Somoe Ng'tu (kulia) na Angela Msangi (kushoto)  
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi kulia akiwa na Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa



    Katika sherehe hizo za jana, Rais Kikwete alikabidhiwa tuzo na TASWA kumshukuru kwa mchango wake mkubwa michezoni kwa kipindi cha miaka 10 ya utawala wake.
    Aidha, naye Rais huyo kipenzi cha Watanzania alikabidhi tuzo kwa Wanamichezo 10 waliofanya vizuri wakati wa utawala wake. Rais pia alikabidhi tuzo kwa viongozi mbalimbali waliofanya vizuri pamoja na wafanyabiashara na asasi zilizomuunga mkono katika kupiga jeki maendeelo ya michezo nchini.
    Wanamichezo waliopata tuzo ni Wanariadha Samson Ramadhan aliyepata Medali ya Dhahabu mwaka 2006 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, Martin Sule aliyepata Medali ya Fedha katika Michezo ya Afrika mwaka 2007 na Mary Naali aliyepata Medali ya Shaba mwaka 2008.
    Kikosi cha Taifa Stars kilichocheza CHAN ya kwanza mwaka 2009 kilipata tuzo, mchezaji Nitiboli Mwanaidi Hassan, bondia Francis Cheka, kocha Charles Boniface Mkwasa kwa kuiwezesha timu ya wanawake, Twiga Stars kucheza fainali za Afrika na mshambuliaji Mbwana Samatta kwa mafanikio yake TP Mazembe wote walipokea tuzo.
    Upande wa viongozi Jenerali Mstafu Waitara kwa kujenga Uwanja wa Gofu, Kanali Mstaafu Iddi Kipingu kwa uwekezaji wake katika michezo ya vijana, Dioniz Malinzi kwa kujenga Uwanja wa Gofu Bukoba, Leodegar Tenga kwa kuifanya TFF kuwa taasisi yenye kuheshimika na Mtangazaji Abdallah Majura kwa kuweza kuanzisha kituo chake mwenyewe cha Redio (ABM).
    Makampuni na wadau waliopewa tuzo ni pamoja na Bakhresa Limited kwa mchango wao mkubwa michezoni na TSN pia.     
    Rais Kikwete aliyeiongoza nchi tangu mwaka 2005, anamaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu na anatarajiwa kukabidhi madaraka baada ya uchaguzi Mkuu mapema mwezi ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS KIKWETE: WATU WANAPENDA ‘MISIFA’ YA KUITWA RAIS, MWENYEKITI LAKINI HAWASAIDII CHOCHOTE MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top