Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI wa kimataifa wa Burundi, Emery Nimubona anayecheza pembeni kulia na kushoto, atakuwa nje ya kikosi cha klabu yake, Simba SC kwa wiki nne, kufuatia kuumia kidole cha mkono wa kushoto.
Nimubona aliumia wiki hii mazozini Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na baada ya vipimo, imegundulika atahitaji wiki nne za mapumziko.
Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba Nimubona atahitaji wiki nne za mapumziko baada ya kuumia kidole hicho na baada ya hapo ataanza mazoezi.
“Nimubona amevunjika kidole cha mkono wa kushoto wakati akiwa nafanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbeya City na tayari amefungwa plasta gumu (PoP),”amesema.
Simba SC inaendelea na mazoezi yake kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbeya City mjini Mbeya Oktoba 17, mwaka huu.
Na Nimubona anaungana na mchezaji mwingine wa kigeni, mshambuliaji Mganda Hamisi Kizza ‘Diego’ aliyeumia nyama za paja wiki iliyopita mazoezini pia.
Lakini Kizza anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi Jumatatu na kama hali yake itaendelea kuimarika vizuri, basi kocha Muingereza Dylan Kerr atamuingiza kwenye programu za mechi na Mbeya City.

Emery Nimubona anatarajiwa kuwa nje kwa wiki nne baada ya kuumia wiki hii |
“Nimubona amevunjika kidole cha mkono wa kushoto wakati akiwa nafanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbeya City na tayari amefungwa plasta gumu (PoP),”amesema.
Simba SC inaendelea na mazoezi yake kujiandaa na mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbeya City mjini Mbeya Oktoba 17, mwaka huu.
Na Nimubona anaungana na mchezaji mwingine wa kigeni, mshambuliaji Mganda Hamisi Kizza ‘Diego’ aliyeumia nyama za paja wiki iliyopita mazoezini pia.
Lakini Kizza anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi Jumatatu na kama hali yake itaendelea kuimarika vizuri, basi kocha Muingereza Dylan Kerr atamuingiza kwenye programu za mechi na Mbeya City.
0 comments:
Post a Comment