// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NDEMLA AANZA LEO STARS NA MALAWI, MKWASA APANGA KIKOSI CHA ‘HATOKI MTU’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NDEMLA AANZA LEO STARS NA MALAWI, MKWASA APANGA KIKOSI CHA ‘HATOKI MTU’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 07, 2015

    NDEMLA AANZA LEO STARS NA MALAWI, MKWASA APANGA KIKOSI CHA ‘HATOKI MTU’

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amemuanzisha kiungo wa Simba SC, Said Hamisi Ndemla katika kikosi kitakachomenyana na Malawi jioni ya leo mechi ya mchujo wa awali Kombe la Dunia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ndemla ameanza badala ya kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya, ambaye leo anaanzia benchi.
    Ndemla alikuwa mchezaji pekee wa Simba SC kucheza katika kikosi cha Stars kilichotoa sare ya 0-0 na Nigeria Septemba 5, mwaka huu baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Mudathir dakika ya 61.
    Said Ndemla (kushoto) anaanza pamoja na Mwinyi Mngwali (kulia)

    Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco aliyeingia dakika ya 67 siku hiyo kuchukua bafasi ya Mrisho Ngassa leo hayupo hata benchi kwa sababu ni majeruhi na badala yake ameketi Ibrahim Hajib.
    Kwa ujumla Mkwasa amerudi na kikosi kile kile kilichotoa sare ya 0-0 na Super Eagles katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, kasoro Mudathir tu.
    Kikosi kamili cha Stars kitakuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Said Ndemla, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Farid Mussa.
    Malawi; Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone, Chawangiwa Kawanda, John Banda na Robin Ngalande.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDEMLA AANZA LEO STARS NA MALAWI, MKWASA APANGA KIKOSI CHA ‘HATOKI MTU’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top