Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA maarufu nchini, Juma Mwambusi (pichani kushoto) ameaga rasmi leo katika klabu yake, Mbeya City na kesho anatarajiwa kutambulishwa kesho kuwa kocha mpya wa Yanga SC ya Dar es Salaam.
Mwambusi amewaachia simanzi viongozi wa Mbeya City, timu ambayo aliipandisha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 na kuwa tishio nchini ndani ya muda mfupi.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba ni kweli Mwambusi ameaga, lakini hajasema anaelekea wapi.
Kimbe hakutaka kueleza zaidi juu ya kocha wao huyo anakokwenda kujiunga katika kazi yake hiyo, lakini ni wazi anakwenda Yanga SC ambako amepata dau zuri.
Yanga SC imefikia makubaliano na Mwambusi, kocha wa zamani wa Moro United akachukue nafasi ya Charles Boniface Mkwasa aliyekuwa Msaidizi wa Mholanzi, Hans van der Pluijm.
Mkwasa amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kufundisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na tayari ameaga Yanga SC.
Kwa sababu hiyo, mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wanataka mbadala wa Mkwasa haraka iwezekanavyo na rada zao zimemlenga Mwambusi.
BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE inafahamu baada ya mchakato wa kupitia majina kadhaa yaliyopendekezwa, jina la Mwambusi lilipita bila ya kipingamizi hususan kutokana na kupendekezwa pia kocha Mkuu, Pluijm.
Mambo matatu yamempa ulaji Mwambusi Yanga SC, ni muadilifu, mchapakazi na hana majungu.

0 comments:
Post a Comment