Na Princess Asia, BLANTYRE
KOCHA Mkuu wa Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba ana matumaini ya ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Malawi.
Taifa Stars leo inashuka Uwanja wa Kamuzu mjini hapa kumenyana na wenyeji Malawi katika mchezo wa marudiano hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwnaia tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi.
Na wakati timu hiyo inahitaji hata sare ili kusonga mbele baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam Jumatano, kocha Mkwasa amesema; “Tunaweza kushinda,”.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE Mkwasa amesema kwamba ataanzisha washambuliaji wake wote hatari Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ili kuwaogopesha wenyeji wao.
“Tutacheza kwa tahadhari lazima, lakini tutashambulia moja kwa moja. Na kwa kiasi kikubwa tuna matumaini ya kushinda hata hapa,”amesema.
Kwa upande wake, kocha Ernest Mtawali amesema kwamba amekiandaa vizuri kikosi chake kwa mchezo wa marudiano na ana matumaini ya kupindua matokeo na kuitoa Tanzania.
“Tumefanyia kazi makosa, tumejiandaa vizuri na vijana wako vizuri kuelekea mchezo huo. Kama wao walitufunga 2-0 kwao, na sisi tutashinda hapa kwetu 3-0 na kuwatoa,”amesema kiungo huyo wa zamani wa Newell's Old Boys ya Argentina na Toulouse FC ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa mazoezi ya Stars jana, inavyoonekana leo Mkwasa ataanza na viungo watatu wa kati, Himid Mao, Said Ndemla na Mudathir Yahya, wakati mmoja kati ya Mrisho Ngassa au Farid Mussa anaweza kuanzia benchi.
Hakutarajiwi kuwa na mabadiliko katika safu ya ulinzi, Ally Mustafa ‘Barthez’ akitarajiwa kuendelea kusimama langoni, akilindwa na Shomary Kapombe kulia, Mwinyi Mngwali kushoto, Kelvin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katikati.
Na mbele, Mkwasa anayeshirikiana na Msaidizi wake, Hemed Morocco na Mshauri wake, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ atawaanzisha Samatta na Ulimwengu na ama Ngassa au Farid.
Mshambuliaji mwingine mkali wa mabao Taifa Stars, John Bocco aliyekosa mechi ya kwanza kutokana na kuwa majeruhi amepona na amefanya mazoezi na timu tangu ilipowasili hapa juzi jioni. Wachezaji wote wanaonekana wapo vizuri kuelekea mchezo huo ambao matokeo yake yanawaweka ‘roho juu’ Watanzania nyumbani.
Watanzania wanaweza kupata fursa ya kuushuhudia moja kwa moja mchezo huo kupitia king’amuzi cha Azam TV katika chaneli ya Malawi TV kuanzia Saa 9:00 Alasiri kwa saa za nyumbani.
Mshindi wa jumla atasonga mbele ambako atamenyana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo. Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania. Amin.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ana matumaini ya ushindi ugenini leo dhidi ya Malawi |

Wachezaji wa Taifa Stars katika mazoezi ya jana Uwanja wa Kamuzu jana mchana |
Na mbele, Mkwasa anayeshirikiana na Msaidizi wake, Hemed Morocco na Mshauri wake, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ atawaanzisha Samatta na Ulimwengu na ama Ngassa au Farid.
Mshambuliaji mwingine mkali wa mabao Taifa Stars, John Bocco aliyekosa mechi ya kwanza kutokana na kuwa majeruhi amepona na amefanya mazoezi na timu tangu ilipowasili hapa juzi jioni. Wachezaji wote wanaonekana wapo vizuri kuelekea mchezo huo ambao matokeo yake yanawaweka ‘roho juu’ Watanzania nyumbani.
Watanzania wanaweza kupata fursa ya kuushuhudia moja kwa moja mchezo huo kupitia king’amuzi cha Azam TV katika chaneli ya Malawi TV kuanzia Saa 9:00 Alasiri kwa saa za nyumbani.
Mshindi wa jumla atasonga mbele ambako atamenyana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo. Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania. Amin.
0 comments:
Post a Comment