// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MKWASA AWAONGEZA BUSUNGU NA MAGURI TAIFA STARS, KIKOSI KWENDA OMAN NOVEMBA 1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MKWASA AWAONGEZA BUSUNGU NA MAGURI TAIFA STARS, KIKOSI KWENDA OMAN NOVEMBA 1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 27, 2015

    MKWASA AWAONGEZA BUSUNGU NA MAGURI TAIFA STARS, KIKOSI KWENDA OMAN NOVEMBA 1

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewaongeza kikosini washambuliaji Malimi Busungu wa Yanga SC na Elias Maguri katika kikosi kitakachomenyana na Algeria katikati ya mwezi ujao.
    Taifa Stars itamenyana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 Urusi, baada ya kuitoa Malawi katika hatua ya kwanza. 
    Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam, Mkwasa ametaja wachezaji 28 ambao watakwenda kambini Oman Novemba 2, mwaka huu.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari leo hoteli ya Serena. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars, Farough Baghozah

    Mkwasa amewataja wachezaji hao kuwa ni makipa; Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). 
    Mabeki ni Shomary Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan (Yanga SC), Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka (Simba SC) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar). 
    Viungo ni Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude, Said Ndemla (Simba SC) na Salum Telela (Yanga SC).
    Washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Free State Stars, A. Kusini), Farid Mussa, John Bocco (Azam FC), Simon Msuva, Malimi Busungu (Yanga SC), Elias Maguri (Stand United) na Ibrahim Hajib (Simba SC).
    Mkwasa amesema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 1 katika hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam kabla ya safari ya Muscat, Oman kwa kambi ya siku 10. 
    Amesema wakiwa Oman, pamoja na mazoezi, watacheza mchezo mmoja au miwili ya kujipima na wenyeji wao, iwapo watakuwa tayari kabla ya kurejea Dar es Salaam Novemba 11 tayari kwa mchezo wa kwanza na Algeria Novemba 14, Uwanja wa Taifa.
    Amesema kikosi kitaondoka Dar es Salaam kwenda Algiers Novemba 16, tayari kwa mchezo wa marudiano Novemba 17. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA AWAONGEZA BUSUNGU NA MAGURI TAIFA STARS, KIKOSI KWENDA OMAN NOVEMBA 1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top