Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba anahitaji wachezaji wapya wanne bora kuongeza katika timu yake kabla ya mchezo na Algeria.
Tanzania imeitoa Malawi katika hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 nyumbani na juzi kufungwa 1-0 Blantyre.
Na baada ya matokeo hayo, Taifa Stars itamenyana na Algeria katika hatua ya mwisho ya mchujo, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam Novemba 14 na marudiano Novemba 17 Algiers.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE mjini Dar es Salaam jana baada ya timu kurejea kutoka Malawi, Mkwasa amesema anahitaji beki wa kati mmoja, kiungo wa ulinzi, kiungo mchezeshaji na mshambuliaji.
Amesema wachezaji hao atawatafuta katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na atalazimika kutazama mechi tofauti kaunzia sasa kutafuta anachokitaka.
“Nitaangalia kwenye mechi tofauti, sitachagua mtu kwa sababu amecheza vizuri mechi moja, nitamchukua mtu baada ya kujiridhisha uwezo wake kwa ujumla,”amesema.
Mkwasa, ambaye ni kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, amesema ataangalia pia takwimu za mchezaji ili kujiridhisha zaidi juu ya uwezo wake.
“Kama mtu anafunga mabao kaunzia manne ndani mechi sita na si ya penalti, katika nafasi ya ushambuliaji, huyo ninaweza kumpa nafasi ili kuona uwezo wake zaidi, namna ya uchezaji wake, uelewa wake wa mpira, akiwa na mpira na akiwa hana anafanyeje,”amesema.
MUDA WA MAANDALIZI DHIDI YA ALGERIA MFUPI
Aidha, Mkwasa amesema muda wa maandalizi uliopangwa kuelekea mchezo na Algeria ni mfupi, hivyo amepanga kukutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuangalia uwezekano wa kuongeza muda.
“Kwa mujibu wa kalenda, wanataka kambi ya mechi na Algeria iwe Novemba 9, wakati mechi yenyewe (ya kwanza) ni Novemba 14 (Dar es Salaam), maana yake tuna siku nne tu za maandalizi kabla ya mechi. Hizi ni chache sana,”amesema Mkwasa.
Mkwasa amesema ataishauri TFF kuahirisha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania za timu ambazo zinatoa wachezaji wengi timu ya taifa, ambazo kwa kawaida huwa ni Azam FC, Simba na Yanga SC.
“Nitashauri mechi zao (Azam FC, Simba na Yanga) ambazo zimepangwa kuchezwa Novemba 7 ziahirishwe, ili zichezwe kabla ya Kombe la Challenge, ili tupate muda mrefu kidogo wa maandalizi kabla ya mechi na Algeria,” amesema Mkwasa.
Mechi za Ligi Kuu Novemba 17 ni Mgambo Vs Yanga SC mjini Tanga, Kagera Sugar Vs Ndanda FC mjini Tabora, Stand United Vs Mwadui FC mjini Shinyanga, Mbeya City Vs Mtibwa Sugar mjini Mbeya, Azam FC Vs Simba SC mjini Dar es Salaam na Majimaji FC Vs Toto Africans mjini Songea.
Novemba 8, raundi hiyo itahitimishwa kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Prisons mjini Dar es Salaam, Coastal Union Vs African Sports mjini Tanga, kabla ya mapumziko ya maandalizi ya mchezo na Algeria Novemba 9 Dar es Salaam hadi Novemba 17.
Baada ya hapo kutakuwa na mapumziko ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Challenge kuanzia Novemba 15 hadi Desemba 15.
MTAZAMO WAKE KUHUSU ALGERIA
Mkwasa pia aliwazungumzia wapinzani wake wajao, Algeria na akakiri ni timu kubwa na nzuri yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa na wanaocheza Ulaya.
Amesema Algeria ndiyo timu bora kwa sasa Afrika, hivyo anafahamu fika anaingia kwenye mtihani mgumu ndiyo maana anataka maandalizi ya kutosha.
“Algeria wana falsafa zao za mpira, na haziko sawa. Wana falsafa tofauti ya uchezaji kutegemea na wapinzani wao. Wakicheza na Libya ni tofauti na watakapocheza na Tanzania. Wanabadilika badilika, ila nashukuru tu kujua aina ya uchezaji wao, inatosha,”amesema.
Mkwasa amesema yanahitajika maandalizi ya kutosha kabla ya mchezo huo, ikiwezekana apatiwe na mechi moja ya majaribio dhidi ya wapinzani kutoka Kaskazini.
“Hata tukipata mechi na Sudan, itatusaidia, kwa sababu michezo yao inafanana fanana, nitakutana na viongozi wa TFF tutajadili kuhusu maandalizi,”amesema.
Kuhusu Taifa Stars kwa ujumla, Mkwasa aliyerithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij Julai mwaka huu, amesema kwamba ana kazi kubwa, kwa maana ya kuirudisha timu katika kiwango chake na kurejesha imani ya wapenzi.
“Natakiwa kujenga timu imara ndani ya muda mfupi na hilo si jambo jepesi, kwa sababu hatuna wigo mpana sana wa wachezaji wa kiwango cha kimataifa, ila kwa kushirikiana na wenzangu, tutajitahidi,”amesema.

Charles Boniface Mkwasa 'Master' anataka wachezaji wanne wapya Taifa Stars |

Kikosi cha Taifa Stars kilichoitoa Malawi hatua ya kwanza ya mchujo Kombe la Dunia |
MTAZAMO WAKE KUHUSU ALGERIA
Mkwasa pia aliwazungumzia wapinzani wake wajao, Algeria na akakiri ni timu kubwa na nzuri yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa na wanaocheza Ulaya.
Amesema Algeria ndiyo timu bora kwa sasa Afrika, hivyo anafahamu fika anaingia kwenye mtihani mgumu ndiyo maana anataka maandalizi ya kutosha.
“Algeria wana falsafa zao za mpira, na haziko sawa. Wana falsafa tofauti ya uchezaji kutegemea na wapinzani wao. Wakicheza na Libya ni tofauti na watakapocheza na Tanzania. Wanabadilika badilika, ila nashukuru tu kujua aina ya uchezaji wao, inatosha,”amesema.
Mkwasa amesema yanahitajika maandalizi ya kutosha kabla ya mchezo huo, ikiwezekana apatiwe na mechi moja ya majaribio dhidi ya wapinzani kutoka Kaskazini.
“Hata tukipata mechi na Sudan, itatusaidia, kwa sababu michezo yao inafanana fanana, nitakutana na viongozi wa TFF tutajadili kuhusu maandalizi,”amesema.
Kuhusu Taifa Stars kwa ujumla, Mkwasa aliyerithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij Julai mwaka huu, amesema kwamba ana kazi kubwa, kwa maana ya kuirudisha timu katika kiwango chake na kurejesha imani ya wapenzi.
“Natakiwa kujenga timu imara ndani ya muda mfupi na hilo si jambo jepesi, kwa sababu hatuna wigo mpana sana wa wachezaji wa kiwango cha kimataifa, ila kwa kushirikiana na wenzangu, tutajitahidi,”amesema.
0 comments:
Post a Comment