// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MIKAKATI YA ‘KUITOA NISHAI’ ALGERIA YAANZA MARA MOJA CHINI YA KAMATI YA TAIFA STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MIKAKATI YA ‘KUITOA NISHAI’ ALGERIA YAANZA MARA MOJA CHINI YA KAMATI YA TAIFA STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 15, 2015

    MIKAKATI YA ‘KUITOA NISHAI’ ALGERIA YAANZA MARA MOJA CHINI YA KAMATI YA TAIFA STARS

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya kusaidia timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanya kikao chake cha kwanza usiku wa leo, kujadili mwanzo wa kazi zao.
    Kamati hiyo iliyotajwa leo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi imekutana katika hoteli ya New Africa mjini Dar es Salaam usiku wa leo.
    Chini ya Mwenyekiti wake Farouqh Baghozah, jukumu la kwanza la Kamati hiyo iliyopewa jina Kamati ya Taifa Stars ni kuisaidia timu hiyo katika mechi zake mbili dhidi ya Algeria mwezi ujao.
    Taifa Stars inamenyana na Algeria, mwezi ujao katika hatua ya mwisho ya mchujo ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2016 Urusi.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars, Farough Baghozah (kushoto) akimsikiliza Mjumbe wake, Michael Wambura wakati wa kikao chao usiku huu hoteli ya New Africa, Dar es Salaam
    Baghozah (katikati) akisikiliza hoja za Wajumbe
    Mikakati mizito inapangwa kuhakikisha Algeria inag'olewa
    Kulia ni Juma Pinto na kushoto Ahmed Iddi Mgoyi, maarufu kwa jina la Msafiri
    Kulia Baraka Kizuguto, ambaye ni Ofisa Habari wa TFF na kushoto Katibu wa Kamati, Teddy Mapunda
    Wakili Imani Madega (kushoto) naye alikuwepo kwenye kikao hicho cha kwanza 


    Hiyo inafuatia kuitoa Malawi ‘Mwale’ katika hatua ya kwanza ya mchujo kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 nyumbani na Jumapili kufungwa 1-0 Blantyre.
    Mechi ya kwanza na Algeria itachezwa Dar es Salaam Novemba 14 na marudiano Novemba 17 Algiers.
    Na katika kuimarisha maandalizi ya timu, Malinzi ameunda kamati maalum ambayo majukumu yake  ni kuimarisha huduma kwa wachezaji, uhamasishaji na masoko, kuhamasisha wachezaji na kuandaa na kusimamia mikakati ya ushindi.
    Mapema leo, Malinzi amesema Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
    Lakini katika kikao cha leo, kulikuwa kuna Wajumbe ambao hawakutajwa na Malinzi wakati wa kuitambulisha Kamati hiyo, akiwemo mfanyabishara maarufu, Mussa Katabaro. 
    Aidha, Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.
    Malinzi ameomba wadau wa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika kamati hiyo waitikie wito huo.
    Algeria, timu namba moja kwa ubora wa soka Afrika na namba 19 duniani, inaonekana ‘kumnyima usingizi’ kila Mtanzania, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamaliza muda wake Oktoba 25.
    Akizungumza katika hafla ya kupongezwa kwake na Wanamichezo Jumatatu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Rais Kikwete alisema kwamba Algeria ni timu nzuri.
    Alisema Algeria ndiyo timu ya Afrika iliyofanya vizuri zaidi ya zote kati ya zilizoshiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka jana Brazil, nyingine zikiwa ni Ivory Coast, Ghana, Nigeria na Cameroon.
    Kwa sababu hiyo, Rais Kikwete amesema huo ni mtihani mgumu kwa Taifa Stars, ingawa ameitakia kila la heri timu hiyo kuelekea mchezo huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MIKAKATI YA ‘KUITOA NISHAI’ ALGERIA YAANZA MARA MOJA CHINI YA KAMATI YA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top