TIMU ya Mbeya City imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa kuhitimisha mzunguko wa tano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya ifikishe pointi nne baada ya mechi tano, ikishinda moja, kufungwa tatu na kutoa sare moja, wakati Toto inafikisha pointi sita, baadaya sare tatu, ushindi mmoja na kufungwa moja.
Mbeya City inayofundishwa na Juma Mwambusi, ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata dakika ya 12 kupitia kwa Jacob Mahundi, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Edward Christopher kuisawazishia Toto ya kocha John Tegete dakika ya 74.
Katika mechi za jana, mabingwa watetezi, Yanga SC waliendelea kung’ang’ania usukani wa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Majimaji FC ilitoka sare ya 1-1 na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji, Songea, Prisons ilitoka 0-0 na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Simba SC imeshinda 1-0 dhidi ya Stand United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mbeya City imelazimishwa sare ya 1-1 na Toto Africans mjini Mwanza |
Mbeya City inayofundishwa na Juma Mwambusi, ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata dakika ya 12 kupitia kwa Jacob Mahundi, kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Edward Christopher kuisawazishia Toto ya kocha John Tegete dakika ya 74.
Katika mechi za jana, mabingwa watetezi, Yanga SC waliendelea kung’ang’ania usukani wa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Majimaji FC ilitoka sare ya 1-1 na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji, Songea, Prisons ilitoka 0-0 na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Simba SC imeshinda 1-0 dhidi ya Stand United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment