// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAGURI AENDELEA ‘KUWACHOMA ROHO’ SIMBA, APIGA MBILI STAND UTD YAUA 3-0 SHINYANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAGURI AENDELEA ‘KUWACHOMA ROHO’ SIMBA, APIGA MBILI STAND UTD YAUA 3-0 SHINYANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Wednesday, October 21, 2015

        MAGURI AENDELEA ‘KUWACHOMA ROHO’ SIMBA, APIGA MBILI STAND UTD YAUA 3-0 SHINYANGA

        MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
        Oktoba 21, 2015
        Yanga SC 4-1 Toto Africans
        Stand United 3-0 Majimaji FC
        JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
        Prisons 1-0 Simba SC
        Coastal Union 1-0 Kagera Sugar
        Kesho; Oktoba 22, 2015
        Ndanda FC Vs Azam FC
        Mwadui FC Vs Mgambo Shooting
        Mbeya City Vs African Sports
        JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
        Elias Maguri aliachwa Simba SC eti anakosa sana mabao, lakini sasa anafunga sana Stand United

        MSHAMBULIAJI Elias Maguri amezidi ‘kumsuta’ kocha Muingereza wa Simba SC, Dylan Kerr baada ya leo kufunga mabao mawili timu yake, Stand United ikishinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. 
        Mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, Maguri amefunga mabao mawili dakika za 47 na 60 timu yake, bao lingine likifungwa na Pastory Athanas dakika ya 66.
        Na Maguri sasa anafikisha mabao nane katika mechi nane za timu yake, akicheza saba tu, mchezo aliokosa ni dhidi ya Simba SC Dar es Salaam Stand ikilala 1-0. 
        Kocha alipendekeza Maguri aachwe katika usajili wa Simba SC msimu huu akidai eti anapoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.
        Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Yanga SC imeifunga 4-1 Toto Africans, Prisons imeifunga 1-0 Simba SC na Coastal Union imeilaza 1-0 Kagera Sugar.
        Ligi Kuu itaendelea kesho, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Ndanda FC na Azam FC Mtwara, Mwadui FC na Mgambo Shooting Shinyanga na Mbeya City na African Sports Tanga.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MAGURI AENDELEA ‘KUWACHOMA ROHO’ SIMBA, APIGA MBILI STAND UTD YAUA 3-0 SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry