MJERUMANI Jurgen Klopp anatarajiwa ikutambulishwa Ijumaa kuwa kocha mpya wa Liverpool, kufuatia kufukuzwa kwa Brendan Rodgers.
Mazungumzo yamekuwa yakifanyika na washauri wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 tangu Jumapili na Liverpool wanajiamini mno kwamba watampata kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.
Mkataba bado haujasainiwa, lakini inatarajiwa kwamba Klopp atapewa isiyopungua miaka mitatu na kampuni ya Fenway Sports Group, wamiliki wa Liverpool kama ambavyo walifanya kwa watangulizi wake, Kenny Dalglish na Brendan Rodgers.
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Jugern Klopp amekuwa kwenye rada za Fenway Sports Group, wamiliki wa Liverpool arithi mikoba ya Rodgers
Klopp amekuwa kwenye rada za FSG ili achukua nafasi ya Rodgers a mipango imekuwa ikipelekwa haraka haraka kuhakikisha hawapotezi fursa ya kumpata kocha huyo mwenye hadhi ya juu katika mchezo huo Ulaya.
Anatarajiwa kuwachukua Wasaidizi wake wa muda mrefu, Zelkjo Buvac na Peter Krawietz akafanye nao kazi, ingawa bado mustakabali wa Sean O'Driscoll, Gary McAllister na Pepijn Lijnders, ambao wote waliteuliwa na Rodgers haujajulikana.
0 comments:
Post a Comment