MJERUMANI Jurgen Klopp hamesaini Mkataba wa kufundisha Liverpool na kutakiwa kuifanya klabu hiyo ya England ifanye vizuri katika michuano ya Ulaya.
Taarifa fupi iliyochapishwa katika tovuti ya klabu jioni ya leo imesema kwamba Klopp ndiye mrithi wa Brendan Rodgers aliyefukuzwa Jumapili baada ya sare ya 1-1 na Everton na anatarajiwa kutambulishwa kesho asubuhi katika Mkutano wa Vyombo vya Habari.
Mtaalamu wa soka ya ushindi na mataji, Klopp amesaini mkataba mnono wa misimu mitatu unaomfanya alipwe si chini ya Pauni Milioni 6 kwa mwaka ambao una kipengele cha kurefushwa kwa miezi 12.
Na wamiliki wa Liverpool, kampuni ya Fenway Sports Group, wamemtaka Klopp kurejesha hadhi ya klabu katika ulimwengu wa soka.
Liverpool imemtangaza Jurgen Klopp kuwa kocha wao mpya, baada ya kusaini Mkataba PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MECHI SITA ZA MWANZO ZA KLOPP LIVERPOOL
Okt 17: Tottenham (ugenini) - Ligi Kuu
Okt 22: Rubin Kazan (nyumbani) - Europa League
Okt 25: Southampton (nyumbani) - Ligi Kuu
Okt 28: Bournemouth (nyumbani) - Kombe la Ligi
Okt 31: Chelsea (ugenini) - Ligi Kuu
Nov 5: Rubin Kazan (ugenini) - Europa League
Ndege binafsi iliyomleta kocha mpya wa Liverpool, Klopp ikiwasili Uwanja wa Ndege wa Liverpool leo mchana
Klopp amewasili Merseyside leo mchana baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa John Lennon na ndege binafsi kutoka Dortmund. Katika ndege hiyo ya dakika 90, alikuwa ameongozana na familia yake na Wasaidizi wake anaowaamini Zeljko Buvac na Peter Krawietz.
Sean O'Driscoll na Gary McAllister, makocha walioletwa na Brendan Rodgers msimu huu, wameondolewa leo.
0 comments:
Post a Comment