// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KLOPP APATA 'BONGE LA PIGO' LIVERPOOL, INGS NA GOMEZ WOTE NJE MSIMU MZIMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KLOPP APATA 'BONGE LA PIGO' LIVERPOOL, INGS NA GOMEZ WOTE NJE MSIMU MZIMA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 15, 2015

    KLOPP APATA 'BONGE LA PIGO' LIVERPOOL, INGS NA GOMEZ WOTE NJE MSIMU MZIMA

    KOCHA mpya wa Liverpool, Mjerumani Jurgen Klopp amepata pigo la pili kuelekea mechi yake ya kwanza mwishoni mwa wiki tangu aanze kazi wiki hii, akirithi mikoba ya Brendan Rodgers.
    Hiyo inafuatia kuumia kwa mshambuliaji tegemeo kwa sasa Liverpool, Danny Ings ambaye anaweza kukosekana msimu wote.
    Mpachika mabao huyo ambaye ndiyo kwanza aliichezea kikamilifu England katika mchezo wake wa kwanza Jumatatu nchini Lithuania, ameumia mguu sawa na alivyoumia beki kinda wa pembeni, Joe Gomez alipokuwa akiichezea timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 usiku wa Jumanne.
    Klopp amethibitisha kwamba Gomez atakuwa nje kwa msimu wote wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano wake wa kwanza, Melwood.
    Lakini kwa bahati mbaya zaidi inagundulika kwamba Ings, ambaye amekuwa mchezaji tegemeo wa Liverpool kwa sasa ana matatizo kama hayo yanayotarajiwa kumuweka nje kwa msimu wote.
    Liverpool imepata pigo baada ya kugundulika kwamba mshambuliaji Danny Ings (katikati) atakosa sehemu yote ya msimu iliyobaki PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KLOPP APATA 'BONGE LA PIGO' LIVERPOOL, INGS NA GOMEZ WOTE NJE MSIMU MZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top