Issa Hayatou atakaimu Urais wa FIFA hadi Februari mwakani utakapofanyika uchaguzi |
Hatua hiyo inafuatia kusimamishwa kwa Rais wa FIFA, Sepp Blatter na Rais wa UEFA, Michel Platini kwa siku kutojihusisha kabisa na soka.
Katibu wa FIFA, Jerome Valcke naye pia amesimamishwa kwa siku 90 maana yake watu hao watatu wa nguvu katika ulimwengu wa soka wamesimamishwa wakati uchunguzi wa Kamati ya Maadili ya FIFA unaendelea.
Kifungo hicho kinazima ndoto za Blatter kuendelea kuwa madarakani hadi Februari na kinamkatisha tamaa Rais wa UEFA, Platini kurithi nafasi hiyo mwakani.
Sepp Blatter na Michel Platini wamesimamishwa na Kamati ya Maadili ya FIFA kwa siku 90
Kamati ya Maadili pia imetangaza kwamba mgombea mwingine wa Urais wa FIFA, Chung Mong-joon wa Korea amefungiwa miaka sita na kutozwa faini ya ya fedha za Uswisi 100,000 kwa kuvunja sheria wakati wa kampeni za kuomba uenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.
Hii inafuatia madai ya Pauni Milioni 1.35 alizopokea Platini mwaka 2011 kwa kazi ushauri kwa Blatter miaka tisa iliyotangulia, ambazo hazijatolewa ufafanuzi.
Blatter naye pia anachunguzwa kwa kuuza haki za matangazo ya Televisheni za Kombe la Dunia kwa mshirika wake wa FIFA, Jack Warner kwa bei ya chini ambayo baadaye iligundulika ilimuingizia faida ya Pauni Milioni 11 raia huyo wa Trinidad.
Taarifa ya Kamati ya Maadili ya FIFA imesema; "Kikao cha Kamati ya Maadili kilichoongozwa na Mwenyekiti Hans Joachim Eckert kimemsimamisha Rais wa FIFA, Joseph S. Blatter, Rais wa UEFA na Makamu wa Rais wa FIFA, Michel Platini, na Katibu wa FIFA, Jerome Valcke (ambaye tayari alipewa likizo na mwajiri wake FIFA) kwa siku 90.

0 comments:
Post a Comment