// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIGODEKO AZIMA SHANGWE ZA YANGA KAMBARAGE, AWACHOMOLEA MWADUI DAKIKA ZA LALA SALAMA, SARE 2-2 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIGODEKO AZIMA SHANGWE ZA YANGA KAMBARAGE, AWACHOMOLEA MWADUI DAKIKA ZA LALA SALAMA, SARE 2-2 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 28, 2015

    KIGODEKO AZIMA SHANGWE ZA YANGA KAMBARAGE, AWACHOMOLEA MWADUI DAKIKA ZA LALA SALAMA, SARE 2-2

    MATOKEO NA RATIBA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
    Leo Oktoba 28, 2015
    Toto African 1-0 Mgambo Shooting
    Mwadui FC 2-2 Yanga SC
    Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar
    Mbeya City 1-1 Majimaji Fc Sokoine
    Ndanda FC 0-0 Stand United
    Simba Sc 1-0 Coastal Union
    Oktoba 29, 2015
    Prisons        Vs African Sports
    JKT Ruvu    Vs Azam FC
    Donald Ngoma amefunga mabao yote ya Yanga SC ikitoa sare ya 2-2 na Mwadui

    Na Prince Akbar, SHINYANGA
    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC, Bakari Kigodeko ameipokonya tonge mdomoni Yanga SC jioni ya leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga baada ya kuifungia Mwadui FC bao la kusawazisha dakika la salama timu hizo zikitoka sare ya 2-2.
    Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mzimbabwe Donald Ngoma alifunga mabao yote Yanga SC, moja kila kipindi.  
    Sare hiyo ya pili msimu huu, inawafanya mabingwa hao watetezi wafikishe pointi 20, baada ya mechi nane ingawa wanaendelea kuongoza Ligi Kuu, wakiizidi pointi moja Azam FC, ambayo kesho inacheza na JKT Uwanja wa Karume.   
    Yanga SC ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nane mfungaji Donald Ngoma aliyemalizia pasi ya Mbrazil Andrey Coutinho.
    Mwadui walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 40 kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City, Paul Nonga ambaye mabeki wa Yanga walimuacha wakidhani ameotea.
    Kipindi cha pili, Ngoma alifunga dakika ya 75, kabla ya Kigodeko kuisawazishia Mwadui FC dakika ya 88.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Andrey Coutinho/Simon Msuva dk56, Thabani Kamusoko/Haruna Niyonzima dk80, Malimi Busungu/Deus Kaseke dk56, Amissi Tambwe na Donald Ngoma. 
    Mwadui FC; Shaaban kado, Shaaban Hassan, Malika Ndeule, David Luhende, Emmanuel Simwanda, Joram Mgeveke, Anthony Matogolo, Jamal Mnyate, Jabir Aziz/Athumani Iddi 'Chuji' dk70, Paul Nonga na Rashid Mandawa/Bakari Kigodeko dk67. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIGODEKO AZIMA SHANGWE ZA YANGA KAMBARAGE, AWACHOMOLEA MWADUI DAKIKA ZA LALA SALAMA, SARE 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top