// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HANS POPPE: MBEYA CITY HAWATUNYIMI USINGIZI SIMBA SC, TUTAWAPIGA NJE NDANI SAFARI HII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HANS POPPE: MBEYA CITY HAWATUNYIMI USINGIZI SIMBA SC, TUTAWAPIGA NJE NDANI SAFARI HII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 09, 2015

    HANS POPPE: MBEYA CITY HAWATUNYIMI USINGIZI SIMBA SC, TUTAWAPIGA NJE NDANI SAFARI HII

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hawaihofii hata kidogo Mbeya City kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Oktoba 17, mwaka huu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo, Hans Poppe amesema kwamba safari hii wataifunga Mbeya City katika mechi zote mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    “Mwaka jana walitufunga mechi zote mbili, na sisi mwaka huu tutalipa kisasi kwa kuwafunga Mbeya na baadaye Dar es Salaam. Na hatusemi hivi kwa sababu tunasema tu, hapana. Tunasema kwa sababu Simba SC ya msimu huu ni nzuri, tofauti sana ya msimu uliopita,”amesema.
    Hans Poppe ametamba Simba SC itawapiga Mbeya City nje na ndani

    Simba SC itakuwa mgeni wa Mbeya City Oktoba 17, mwaka huu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya katika mfululizo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Kikosi cha Simba SC, chini ya kocha wake, Muingereza Dylan Kerr kinaendelea na mazoezi yake Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
    Kocha Kerr ana matumaini ya kumpata kinara wake wa mabao, Hamisi Kizza ‘Diego’ ambaye anasumbuliwa na maumivu ya nyama.
    “Kocha alisema maumivu ya Kizza ni wiki mbili, nadhani hadi Oktoba 17, atakuwa tayari kucheza,”amesema Poppe.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPPE: MBEYA CITY HAWATUNYIMI USINGIZI SIMBA SC, TUTAWAPIGA NJE NDANI SAFARI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top