// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ENYEAMA ASTAAFU SOKA YA KIMATAIFA NA KUSEMA MANENO 'MAZITO' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ENYEAMA ASTAAFU SOKA YA KIMATAIFA NA KUSEMA MANENO 'MAZITO' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 08, 2015

    ENYEAMA ASTAAFU SOKA YA KIMATAIFA NA KUSEMA MANENO 'MAZITO'

    KIPA wa muda mrefu wa timu ya taifa Nigeria, Vincent Enyeama (pichani kushoto) amestaafu soka ya kimataifa baada ya kugombana na kocha Sunday Oliseh katika kambi ya Super Eagles nchini Ubelgiji.
    Kipa huyo wa Tai Mkubwa wa Nigeria ametangaza uamuzi wake huo katika ukurasa wake wa Instagram.
    “Nimepigana mapambano mazuri kwa zaidi ya miaka 13. Nimemaliza wajibu wangu. Nimelinda na kuimba wimbo wa taifa hamasa.
    “Yote niliyoyafanya natarajia malipo yake kutoka kwa MUNGU tu kwa miaka yangu 13 ya kulitumikia taifa. Mungu ibariki NIGERIA.
    “Tangu sasa si Nahodha tena wa timu ya wakubwa ya Nigeria. Si kipa tena wa timu hiyo. Najitoa kwenye timu.
    “Sipo tena kwenye majukumu ya kimataifa. Nataka nisema asante kwa kila mshabiki wa Nigeria na wanaoniunga mkono dunia nzima.
    “Kimekuwa kipindi cha majaribu zaidi katika maisha yangu, lakini nafahamu kwamba Wanigeria wapo nami, na Mungu yupo nami,"amesema.
    Oliseh alifukuza Enyeama kwenya kambi ya timu hiyo nchini Ubelgiji kwa ktumia walinzi, baada ya kuchelewa kuingia kambini.
    Kipa huyo namba moja wa Lille ya Ufaransa, inaelezwa alibishana na kocha, kwa kuendelea kueleza sababu za kuchelewa kwake licha ya kuambiwa anyamaze na kuondoka.
    Na kipa huyo alipogoma kuondoka, kocha huyo aliwaita walinzi waje kumfukuza. Pamoja na Enyeama kutaka kujitetea, lakini hakupata fursa hiyo kwa Oliseh.
    Sakata hili liliibuka baada ya kipa huyo kurejea kambini akitoka kwenye mazishi ya mama yake.

    Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) lilithibitisha mtafaruku baina ya wawili hao, lakini wakajaribu 'kupoza poza' wakisema. "Ni kweli kulikuwa kuna kutoelewana kidogo kambini, lakini tatizo hilo limetatuliwa na Enyeama amebaki kambini,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ENYEAMA ASTAAFU SOKA YA KIMATAIFA NA KUSEMA MANENO 'MAZITO' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top