// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ENGLAND YAZIDI KUPAA KUFUZU EURO 2016, HISPANIA NAYO ‘MOTO WA GESI’, UJERUMANI YADUNDWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ENGLAND YAZIDI KUPAA KUFUZU EURO 2016, HISPANIA NAYO ‘MOTO WA GESI’, UJERUMANI YADUNDWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, October 10, 2015

    ENGLAND YAZIDI KUPAA KUFUZU EURO 2016, HISPANIA NAYO ‘MOTO WA GESI’, UJERUMANI YADUNDWA

    MATOKEO KUFUZU EURO 2016
    Jana, Oktoba 9, 2015  
    Moldova 1-2 Urusi
    Hispania 4-0 Luxembourg
    Slovakia 0-1 Belarus
    Uswisi 7-0 San Marino
    Slovenia 1-1 Lithuania
    Montenegro 2-3 Austria
    Macedonia 0-2 Ukraine
    Liechtenstein 0-2 Sweden
    England 2-0 Estonia
    Juzi, Oktoba 8, 2015
    Jamhuri ya Ireland 1-0 Ujrumani
    Romania 1-1 Finland
    Hungary 2-1 Faroe Islands
    Albania 0-2 Serbia
    Ureno 1-0 Denmark
    Scotland 2-2 Poland
    Ireland Kaskazini 3-1 Ugiriki
    Georgia 4- 0 Gibraltar 
    Raheem Sterling (katikati) akiifungia England bao la pili dakika ya 85 PICHA ZAIDI GONGA HAPA


    TIMU ya taifa ya Engand imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 usiku wa jana dhidi ya Estonia
    katika mchezo wa Kundi E kufuzu Euro mwaka huu Uwanja wa Wembley, London.
    Asante kwao wafungaji wa mabao hayo, Theo Walcott dakika ya 45 na Raheem Sterling dakika ya 85 na sasa Three Lions wanafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi tisa na kuzidi kupaa kileleni, wakifuatiwa na Uswisi wenye pointi 18 za mechi tisa pia. 
    Mechi nyingine za kundi hilo jana, Uswisi imeichaoa 7-0 San Marino Uwanja wa AFG Arena mabao ya Michael Lang, Gokhan Inler kwa penalti, 55, Admir Mehmedi, Johan Djourou kwa penalti, Pajtim Kasami, Breel Embolo kwa penalti na Eren Derdiyok. 
    Slovenia imetoka sare ya 1-1 na Lithuania Uwanja wa SRC Stozice, wenyeji wakianza kupata bao kupitia kwa Valter Birsa kwa penalti dakika ya 46 kabla ya Arvydas Novikovas kuisawazishia Lithuani kwa penalti pia dakika ya 79.
    Urusi imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Moldova katika mchezo wa Kundi G, mabao yake yakifungwa na Sergei Ignashevitch dakika ya 58 na Artem Dzyuba dakika ya 78, huku Eugeniu Cebotaru akiwafungia wenyeji dakika ya 85 Uwanja wa Zimbru.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo, Sweden wameshinda 2-0 ugenini dhidi ya Liechtenstein mabao ya Marcus Berg dakika ya 18 na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 55 Uwanja wa Rheinpark.
    Nayo Austria imeshinda 3-2 ugenini dhidi ya Montenegro. Mabao ya Montenegro yamefungwa na Mirko Vucinic dakika ya 32 na Fatos Beqiraj dakika ya 68, wakati ya Austria yamefungwa na Marc Janko dakika ya 55, Marko Arnautovic dakika ya 81 na Marcel Sabitzer dakika ya 90+2 Uwanja wa Podgorica City.

    Mchezaji wa Hispania, David Silva akiangushwa na Lars Gerson katika mchezo dhidi ya Luxembourg jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Hispania imeichapa 4-0 Luxembourg mchezo wa Kundi C Uwanja wa Las Gaunas, mabao ya Santiago Cazorla mawili dakika ya 42 na 85 na Francisco Alcacer Garcia mawili pia dakika ya 67 na 80.
    Mechi nyingine za kundi hilo, Ukraine imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Macedonia mabao yake yakifungwa na Evgen Seleznyov kwa penalti dakika ya 59 na Artem Kravets dakika ya 87 Uwanja wa Filip II Arena, wakati Belarus pia imeshinda 1-0 ugenini dhidi ya Slovakia, bao pekee la Stanislav Dragun dakika ya 34 Uwanja wa Pod Dubnom.
    Mechi za Kundi D juzi, Ujerumani ililala 1-0 ugenini mbele ya Jamhuri ya Ireland, bao pekee la Shane Long dakika ya 70 Uwanja wa Aviva, wakati Scotland imelazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Poland mabao yake yakifungwa na Matt Ritchie dakika ya 45 na Steven Fletcher dakika ya 62, huku Robert Lewandowski akifunga yote ya Poland dakika ya tatu na 90+4.
    Mchezo mwingine wa kundi hilo juzi, Georgia iliitandika 4-0 Gibraltar mabao ya Mate Vatsadze, Tornike Okriashvili kwa penalti, Mate Vatsadze na 
    Valeri Qazaishvili Uwanja wa Boris Paichadze.
    Ureno ilipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Denmark mchezo wa Kundi I, bao pekee la Joao Moutinho dakika ya 66 Uwanja wa Manispaa ya Braga, wakati Serbia imeshinda ugenini 2-0 dhidi ya Albania mabao ya Aleksandar Kolarov dakika ya 90+1 na Adem Ljajic dakika ya 90+4 Uwanja wa Elbasan Arena.
    Ugiriki ilitandikwa 3-1 na Ireland Kaskazini mchezo wa F juzi mabao ya washindi yakifungwa na Steven Davis dakika ya 35 na 58 na Josh Magennis dakika ya 49, wakati la wageni lilifungwa na Christos Aravidis dakika ya 86 Uwanja wa Windsor Park.
    Romania imelazimishwa sare ya 1-1 na Finland
    Ovidiu Hoban, wakati mabao mawili ya Daniel Bode yaliipa Hungary ushindi wa 2-1 dhidi ya Faroe Islands, ambao bao lao lilifungwa na Roaldur Jacobsen Uwanja wa Groupama Arena.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ENGLAND YAZIDI KUPAA KUFUZU EURO 2016, HISPANIA NAYO ‘MOTO WA GESI’, UJERUMANI YADUNDWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top