Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MASHABIKI wa Msanii anayetamba hapa nchini katika Anga ya muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ jana walifunga barabara ya kutoka Uwanja wa Ndege kwa muda wakati Msanii huyo alipowasili.
Diamond aliwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jana akitokea Nchini Marekani alikotwaa tuzo tatu za Afrimma wikiendi ya wiki iliyopita huku akipata mapokezi ya aina yake.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Uwanjani hapo Diamond alisema, atahakikisha hawaangushi mashabiki wake wanaochangia kwa asilimia kubwa kupata tuzo hizo.
Nyota huyo asiyekuwa na mpinzani kwa sasa hapa nchini, alisema kwake yeye ni faraja kubwa, kuona Tanzania inatambulika kupitia yeye, hivyo inampa nafasi ya kuzidi kupambana zaidi na kuitangaza kwani anatambua ana deni kubwa la kuhakikisha anafanya vizuri.
Mara baada ya kuzungumza na wanahabari, Masgabiki hao walianza msafara wakiwa naye na kupelekea kusababisha msongamano mkubwa ulioziba njia kutokana na matembezi hayo.
Mashabiki hao wakiongozwa na kundi lake la Wasafi walianza kuongozana na Diamond wakitembea katikati ya barabara kitendo kilichofanya msongamano mkubwa uliowaradhimu Polisi kuingilia kati.
Baada ya kufika eneo la Vingunguti kwa mguu, baada ya Polisi kufika walimtaka Diamond kusitisha maandamano hayo kwa kupanda gari ili kuepusha msongamano huo, baada ya taarifa hiyo ya Polisi ilimradhimu Diamond kupanda gari la Grobal Publishers huku wafuasi wake wengine wakipanda pikipiki.

Diamond Platinumz akionyesha tuzo zake wakati wa maandamazo ya mapokezi yake leo |
Nyota huyo asiyekuwa na mpinzani kwa sasa hapa nchini, alisema kwake yeye ni faraja kubwa, kuona Tanzania inatambulika kupitia yeye, hivyo inampa nafasi ya kuzidi kupambana zaidi na kuitangaza kwani anatambua ana deni kubwa la kuhakikisha anafanya vizuri.
Mara baada ya kuzungumza na wanahabari, Masgabiki hao walianza msafara wakiwa naye na kupelekea kusababisha msongamano mkubwa ulioziba njia kutokana na matembezi hayo.
Diamond akiwa katikati ya umati wa watu |
Mashabiki hao wakiongozwa na kundi lake la Wasafi walianza kuongozana na Diamond wakitembea katikati ya barabara kitendo kilichofanya msongamano mkubwa uliowaradhimu Polisi kuingilia kati.
Baada ya kufika eneo la Vingunguti kwa mguu, baada ya Polisi kufika walimtaka Diamond kusitisha maandamano hayo kwa kupanda gari ili kuepusha msongamano huo, baada ya taarifa hiyo ya Polisi ilimradhimu Diamond kupanda gari la Grobal Publishers huku wafuasi wake wengine wakipanda pikipiki.
0 comments:
Post a Comment