MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
Oktoba 28, 2015
Toto African Vs Mgambo Shooting
Mwadui FC Vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs Majimaji FC
Ndanda FC Vs Stand United
Simba SC Vs Coastal Union
JKT Ruvu Vs Azam FC
Oktoba 29, 2015
Prisons Vs African Sports
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amesema kwamba ushindani wa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utaendelea kuwa baina yao na Azam FC msimu huu.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jana, Cannavaro amesema kwamba baada ya raundi saba, Azam FC na Yanga SC zinakabana koo tena kileleni.
“Unaweza kujionea mwenyewe, hatujapoteza mechi, na hawajapoteza. Mechi baina yetu tulitoka sare. Sasa sisi tunacheza tukiwafikiria wao, na wao wanacheza wakitufikiria sisi,”amesema.
Cannavaro amesema kwamba wanatambua hawapaswi hata kutoa sare mechi yoyote, zaidi ya kushinda mfululizo iwapo wanataka kuipiku Azam FC katika mbio za ubingwa.
Lakini Cannavaro anatambua kwamba Ligi Kuu ni ngumu kwa sababu timu nyingi ni nzuri, hivyo anawaambia wachezaji wenzake wanatakiwa kujituma kila mchezo.
“Usione tunashinda ukadhani ligi nyepesi, hapana. Ligi ni ngumu sana, isipokuwa sisi kwa sababu tuna malengo tunajituma kila mechi. Wakati mwingine tunacheza na uchovu na maumivu, lakini huwezi kujua,”amesema.
Nahodha huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars pia amesema mfano mchezo uliopita dhidi ya Toto African pamoja na kushinda 4-1, lakini waliingia wakiwa wamechoka kutokana na ugumu wa mchezo dhidi ya Azam FC ulioisha kwa sare ya 1-1.
Yanga SC, ambao ndiyo mabingwa watetezi, wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao dhidi ya Azam FC wakiwa wanalingana kwa pointi, 16 kila mmoja.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa ‘live’ na Azam TV, inatarajiwa kuendelea Jumatano, Yanga SC wakisafiri hadi Shinyanga kwenda kumenyana na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, wakati Azam FC watamenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Toto African watakuwa wenyeji wa Mgambo Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa ndugu zao Kagera Sugar, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji FC Uwanja wa Sokoine, Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Stand United, Simba SC watakuwa wenyeji wa Coastal Union na Alhamisi Prisons watakuwa wenyeji wa African Sports.
Oktoba 28, 2015
Toto African Vs Mgambo Shooting
Mwadui FC Vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs Kagera Sugar
Mbeya City Vs Majimaji FC
Ndanda FC Vs Stand United
Simba SC Vs Coastal Union
JKT Ruvu Vs Azam FC
Oktoba 29, 2015
Prisons Vs African Sports
Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' kulia amesema mbio za ubingwa ni wao na Azam FC |
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ amesema kwamba ushindani wa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utaendelea kuwa baina yao na Azam FC msimu huu.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE jana, Cannavaro amesema kwamba baada ya raundi saba, Azam FC na Yanga SC zinakabana koo tena kileleni.
“Unaweza kujionea mwenyewe, hatujapoteza mechi, na hawajapoteza. Mechi baina yetu tulitoka sare. Sasa sisi tunacheza tukiwafikiria wao, na wao wanacheza wakitufikiria sisi,”amesema.
Cannavaro amesema kwamba wanatambua hawapaswi hata kutoa sare mechi yoyote, zaidi ya kushinda mfululizo iwapo wanataka kuipiku Azam FC katika mbio za ubingwa.
Lakini Cannavaro anatambua kwamba Ligi Kuu ni ngumu kwa sababu timu nyingi ni nzuri, hivyo anawaambia wachezaji wenzake wanatakiwa kujituma kila mchezo.
“Usione tunashinda ukadhani ligi nyepesi, hapana. Ligi ni ngumu sana, isipokuwa sisi kwa sababu tuna malengo tunajituma kila mechi. Wakati mwingine tunacheza na uchovu na maumivu, lakini huwezi kujua,”amesema.
Nahodha huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars pia amesema mfano mchezo uliopita dhidi ya Toto African pamoja na kushinda 4-1, lakini waliingia wakiwa wamechoka kutokana na ugumu wa mchezo dhidi ya Azam FC ulioisha kwa sare ya 1-1.
Yanga SC, ambao ndiyo mabingwa watetezi, wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao dhidi ya Azam FC wakiwa wanalingana kwa pointi, 16 kila mmoja.
Yanga SC FC walitoka sare ya 1-1 wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam |
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa ‘live’ na Azam TV, inatarajiwa kuendelea Jumatano, Yanga SC wakisafiri hadi Shinyanga kwenda kumenyana na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, wakati Azam FC watamenyana na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Toto African watakuwa wenyeji wa Mgambo Shooting Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa ndugu zao Kagera Sugar, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Majimaji FC Uwanja wa Sokoine, Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Stand United, Simba SC watakuwa wenyeji wa Coastal Union na Alhamisi Prisons watakuwa wenyeji wa African Sports.
0 comments:
Post a Comment