WINGA wa Wales, Gareth Bale ni Muingereza pekee aliyepenya katika orodha ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Bale ni miongoni mwa wachezaji 11 wanaocheza Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga walioingia katika orodha hiyo ambayo ina wengine watano wa Ligi Kuu ya England na watano wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga.
Wachezaji watatu wa Manchester City, Sergio Aguero, Kevin De Bruyne na Yaya Toure wameingia kwenye orodha hiyo sambamba na winga wa Chelsea, Eden Hazard na Alexis Sanchez, ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika klabu yake, Arsenal na kuipa mafanikio timu yake ya taifa, Chile katika Copa America mwaka 2015.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale ni Muingereza pekee aliyeingia katika orodha ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mfaransa Arsene Wenger na Mreno Jose Mourinho wote wameingia kwenye 10 bora ya tuzo za kocha bora wa dunia, sambamba na kocha wa mabingwa wa Ulaya, Barcelona Luis Enrique na wa Bayern Munich, Pep Guardiola.
Kocha wa Chile, Jorge Sampaoli ni kocha pekee wa timu ya taifa kwenye orodha hiyo, ambayo pia inahusisha makocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, Unai Emery wa Sevilla, Laurent Blanc wa PSG, Diego Simeone wa Atletico Madrid na Carlo Ancelotti, aliyeondoka Real Madrid baada ya msimu uliopita.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameingia kwenye orodha ya kuwania tuzo ya kocha bora wa mwaka
0 comments:
Post a Comment