// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BAGHOZAH MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA TAIFA STARS, WAJUMBE CHANJI NA MADEGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BAGHOZAH MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA TAIFA STARS, WAJUMBE CHANJI NA MADEGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 15, 2015

    BAGHOZAH MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA TAIFA STARS, WAJUMBE CHANJI NA MADEGA

    KATIKA kuimarisha maandalizi ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) kuelekea katika mashindano mbalimbali ikiwemo mechi mbili za ugenini na nyumbani dhidi ya Algeria, Rais wa TFF Jamal Malinzi ameunda kamati maalum itakayoitwa “Kamati ya Taifa Stars”.
    Malinzi amesema majukumu ya Kamati hiyo yatakua, kuimarisha huduma kwa wachezaji, uhamasishaji na masoko, kuhamasisha wachezaji na kuandaa na kusimamia mikakati ya ushindi.
    Amesema Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Farough Baghouzah, Teddy Mapunda (Katibu), Wajumbe ni Juma Pinto, Michael Wambura, Iman Madega, Salum Abdallah na Isaac Chanji.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars, Farough Baghozah kulia akiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu (kushoto)

    Aidha, Kamati hiyo imepewa jukumu la kuwashirikisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu katika kutekeleza majukumu hayo.
    Malinzi ameomba wadau wa mpira wa miguu ambao kamati itashirikiana nao ili wajumuike na kusaidia majukumu mbalimbali katika kamati hiyo waitikie wito huo.
    Taifa Stars inamenyana na Algeria, mwezi ujao katika hatua ya mwisho ya mchujo ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2016 Urusi.
    Hiyo inafuatia kuitoa Malawi katika hatua ya kwanza ya mchujo kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 nyumbani na Jumapili kufungwa 1-0 Blantyre.
    Mechi ya kwanza na Algeria itachezwa Dar es Salaam Novemba 14 na marudiano Novemba 17 Algiers. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAGHOZAH MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA TAIFA STARS, WAJUMBE CHANJI NA MADEGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top