// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC HATARINI KUMKOSA KAPOMBE MECHI NA YANGA SC JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC HATARINI KUMKOSA KAPOMBE MECHI NA YANGA SC JUMAMOSI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, October 12, 2015

    AZAM FC HATARINI KUMKOSA KAPOMBE MECHI NA YANGA SC JUMAMOSI

    Na Princess Asia, BLANTYRE
    AZAM FC inaweza kumkosa beki wake wa kulia, Shomary Kapombe katika mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi dhidi ya Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hiyo inafuatia Kapombe kuumia jana katika mchezo wa kimataifa kati ya Tanzania na wenyeji Malawi mjini Blantyre.
    Kapombe alimaliza dakika 90 za mchezo huo wa marudiano kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi, lakini akatoka anachechemea.
    Baadaye timu iliporejea katika hoteli ya Malawi Sun, Kapombe alikwenda kufanyiwa uchunguzi na Dk Gilbert Kigadye.
    Shomary Kapombe (kulia) akifanyiwa uchunguzi na Dk Kigadye jana hoteli ya Malawi Sun

    Akizungumzia hali ya mchezaji huyo, Dk Kigadye alisema Kapombe anasumbuliwa na maumivu ya nyayo na ni tatizo la muda.
    “Imekuwa kawaida yake akicheza kwenye Uwanja mgumu tu, anatoka anaumwa nyayo, ila sitarajii athari kubwa, nadhani hata kesho anaweza kuendelea na mazoezi,”amesema.
    Taifa Stars ilifungwa 1-0 na Malawi jana, lakini ikasonga mbele hatua ya mwisho ya mchujo kutokana na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam na sasa itamenyana na Algeria mwezi ujao.
    Kapombe kulia akiwania mpira wa juu dhidi ya mchezaji wa Malawi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC HATARINI KUMKOSA KAPOMBE MECHI NA YANGA SC JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top