RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA WIKI HII
Leo Oktoba 20, 2015
Bayer 04 Leverkusen v Roma Bay
Arsenal v Bayern Munich
Zenit St Petersburg v Lyon
Valencia v KAA Gent
FC Porto v Maccabi Tel Aviv
Dynamo Kyiv v Chelsea
Dinamo Zagreb v Olympiakos
BATE Borisov v Barcelona
Kesho, Oktoba 21, 2015
Juventus v Borussia Monchengladbach
CSKA Moscow v Manchester United
VfL Wolfsburg v PSV
Paris Saint-Germain v Real Madrid
Manchester City v Sevilla
Malmo FF v Shakhtar Donetsk
Galatasaray v Benfica
Atletico de Madrid v FC Astana
KLABU ya Chelsea itawakosa washambuliaji wake Pedro na Loic Remy katika mchezo wa leo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev nchini Ukraine.
Kocha Jose Mourinho amewaambia Waandishi wa Habari jana kwamba wachezaji wote hao wawili wana jajeruhi madogomadogo na itakuwa hatari kuwatumia dhidi ya vinara hao wenza wa Kundi G.
"Wao (Pedro na Remy) wana majeruhi madogo madogo, wote na si maumivu makubwa, lakini hiwezekanikwa wao kucheza, wanacheza katika nafasi ambazo tuna wachezaji mbadala, hivyo hatuwezi kuwatoa mhanga,"amesema Mourinho.
Kocha Jose Mourinho amesafiri hadi Ukraine kuwafuata Dynamo Kiev katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kwa ujumla michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaendelea inaendelea leo, Bayer 04 Leverkusen ikiikaribisha Roma Uwanja wa BayArena mchezo wa Kundi E, Arsenal ikiwa mwenyeji wa Bayern Munich Uwanja wa Emirates mchezo wa Kundi F na Zenit St Petersburg wakiikaribisha Lyon Uwanja wa Petrovski mchezo wa Kundi H.
Mechi nyingine za leo, Valencia CF watakuwa wenyeji wa KAA Gent Uwanja wa Mestalla mchezo wa Kundi H pia, FC Porto watakuwa wenyeji wa Maccabi Tel Aviv Uwanja wa Estadio do Dragao mchezo wa Kundi G, Dinamo Zagreb na Olympiakos Uwanja wa Maksimir mchezo wa Kundi F na BATE Borisov na Barcelona Uwanja wa Borisov Arena mchezo wa Kundi E.
Mechi nyingine zitachewa kesho Juventus wakiikaribisha Borussia Monchengladbach Uwanja wa Juventus mchezo wa Kundi D, CSKA Moscow wakiwa wenyeji wa Manchester United Uwanja wa Arena Khimki mchezo wa Kundi B, VfL Wolfsburg wakiikaribisha PSV Uwanja wa Volkswagen Arena mchezo wa Kundi B pia na Paris Saint-Germain wakiwa wenyeji wa Real Madrid Uwanja wa Parc des Princes mchezo wa Kundi A.
Uwanja wa Etihad, Manchester City wataikaribisha Sevilla mchezo wa Kundi D, Malmo FF wataikaribisha Shakhtar Donetsk Uwanja wa Swedbank mchezo wa Kundi A pia, Galatasaray watakuwa wenyeji wa Benfica Uwanja wa Turk Telekom Arena mchezo wa Kundi C na Atletico Madrid wataikaribisha FC Astana Uwanja wa Vicente Calderon.
Gwiji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry akikimbia kushangilia baada ya kufunga dhidi ya Bayern Munich mwaka 2005
REKODI YA ARSENAL NA BAYERN MUNICH
2000/2001 Ligi ya Mabingwa
Arsenal 2-2 Bayern Munich
Bayern Munich 1-0 Arsenal
2004/2005 Ligi ya Mabingwa
Bayern Munich 3-1 Arsenal
Arsenal 1-0 Bayern Munich
2012/2013 Ligi ya Mabingwa
Arsenal 1-3 Bayern Munich
Bayern Munich 0-2 Arsenal
2013/2014 Ligi ya Mabingwa
Arsenal 0-2 Bayern Munich
Bayern Munich 1-1 Arsenal
0 comments:
Post a Comment