![]() |
Angola imefuzu CHAN ya 2016 baada ya kuitoa Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 |
Baada ya kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Rand wiki iliyopita, Bafana Bafana ilikwenda kupambana kiume ugenini kujaribu kupindua matokeo, lakini bahati haikuwa yao.
Percy Tau alikuwa haba bahati baada ya mpira aliopiga kwa kichwa kuokolewa kwenye mstari, lakini Bafana Bafana wakapata bao karibu na mapumziko, baada ya mabeki wa Angola kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Lyle Lakay, kabla ya Gerson kuwasawazishia wenyeji.
Lakay tena akaifungia Bafana Bafana bao la kipindi cha pili, lakini ni Angola inayofuzu CHAN ya mwakani Rwanda.
0 comments:
Post a Comment