MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero anaweza kukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao, Manchester United wiki mbili zijazo baada ya kuumia nyama akiichezea timu yake ya taifa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliondolewa uwanjani kwa machela Argentina ikifungwa 2-0 na Ecuador usiku wa Alhamisi na viongozi wamesema maumivu hayo ni makubwa.
Aguero bado hajawasili nyumbani kwake mjini Manchester, lakini tayari kuna wasiwasi ndani ya Man City wa kumkosa mpachika mabao wao huyo tegemeo katika mechi dhidi ya mahasimu wao.
Sergio Aguero akiondolewa uwanjani kwa machela katika mchezo wa jana Argentina ikifungwa 2-0 na Ecuador PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment