MATOKEO MECHI ZILIZOMALIZIKA LIGI KUU ENGLAND:
Crystal Palace 2-0 West Bromwich
Norwich City 1-2 Leicester City
Manchester City 6-1 Newcastle United
Aston Villa 0-1 Stoke City
AFC Bournemouth 1-1 Watford
Sunderland 2-2 West Ham United
Muuwaji Sergio Aguero akishangilia baada ya kufikisha mabao matano PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TIMU ya Manchester City imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia kuitandika Newcastle United mabao 6-1 jioni ya leo Uwanja wa Etihad.
Mshambuliaji wa Argentina, Sergio ‘Kun’ Aguero amefunga mabao matano katika ushindi huo dakika za 42, 49, 50, 60 na 63, huku bao lingine la Man City likifungwa Kevin De Bruyne dakika ya 53.
Bao pekee la Newcastle, limefungwa na Mserbia Aleksandar Mitrovic dakika ya 18 na sasa City inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi nane, mbili zaidi ya Manchester United waliocheza mechi saba.
Mechi nyingine za Ligi Kuu zilizomalizika Crystal Palace imeshinda 2-0 dhidi ya West Bromwich, Leicester City imefungwa 2-1 nyumbani na Norwich City, Aston Villa imefungwa 1-0 nyumbani na Stoke City, AFC Bournemouth imelazimishwa sare ya 1-1 na Watford, Sunderland imetoka 2-2 na West Ham United.
Mchezo kati ya mabingwa watetezi, Chelsea na Southampton unaendelea hivi sasa timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 hadi mapumziko.
0 comments:
Post a Comment