// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YAZIDI KUTIMUA VUMBO LIGI KUU, YAITANDIKA JKT 4-1, SALAMU ZAO MSIMBAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YAZIDI KUTIMUA VUMBO LIGI KUU, YAITANDIKA JKT 4-1, SALAMU ZAO MSIMBAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 19, 2015

    YANGA SC YAZIDI KUTIMUA VUMBO LIGI KUU, YAITANDIKA JKT 4-1, SALAMU ZAO MSIMBAZI

    MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA LEO
    Stand United 2-0 African Sports 
    Mgambo Shooting 1-0 Majimaji FC
    Prisons 1-0 Mbeya City
    Yanga SC 4-1 JKT Ruvu
    Kesho Septemba 20, 2015
    Mwadui FC Vs Azam FC
    Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
    Simba SC Vs Kagera Sugar
    Coastal Union Vs Toto Africans
    Donald Ngoma akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Yanga SC leo Uwanja wa Taifa

    Na Prince Akbar, DAR ES ALAAM
    YANGA SC imetoa onyo kwa mahasimu wao, Simba SC kuelelea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuwatandika JKT Ruvu mabao 4-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ushindi huo wa tatu mfululizo unaifanya Yanga SC itimize pointi tisa na kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV. 
    Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 30 akimalizia pasi fupi ya Amissi Tambwe baada ya kazi nzuri ya kiungo wa kulia Deus Kaseke.
    Yanga SC ilitawala mchezo kipindi cha kwanza, lakini haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, wakati JKT walicheza kwa kujihami zaidi kipindi hicho.
    Kipindi cha pili, Yanga SC walirudi na kasi ya kusaka mabao zaidi na iliwachukua dakika tatu tu kupata bao la pili, lililofungwa na Mrundi, Amissi Tambwe aliyemalizia krosi ya Kaseke.
    JKT wakafanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 49, kupitia kwa beki na Nahodha wake, Geogre Minja aliyetumia mwanya wa wachezaji wa Yanga SC kuzubaa baada ya kupata bao la pili.
    Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara misimu miwili iliyopita, Amissi Tambwe akaifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 62 kwa kichwa akimalizia krosi ya Simon Msuva.  
    Kiungo wa Yanga SC, Deus Kaseke akienda chini baada ya kukwatuliwa na beki wa JKT Ruvu, Emmanuel Pius


    Mfungaji wa bao la nne Yanga SC, Thabani Kamusoko akimtoka kiungo wa JKT Ruvu, Samuel Kamuntu

    Donald Ngoma akimtoka beki wa JKT Ruvu, George Minja 

    Mfungaji wa mabao mawili ya Yanga SC, Amissi Tambwe akiwatoka mabeki wa JKT Ruvu 

    Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akahitimisha sherehe za mabao Yanga SC kwa kufunga bao la nne, dakika ya 87 kwa shuti la nje ya boksi baada ya kukutana na mpira uliookolewa na Michael Aidan kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Mbuyu Twite baada ya Msuva kuangushwa.
    Katika mechi nyingine za ligi hiyo jioni ya leo, Stand United imeshinda 2-0 dhidi ya African Sports ya Tanga Uwanja wa Kambarage, Shinyanga mabao yote yakifungwa na Elias Maguri, wakati Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee Fully Maganga limeipa Mgambo Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Majimaji FC na Uwanja wa Sokoine, Mbeya Prisons imeshinda 1-0 dhidi ya Mbeya City bao pekee la Jumanne Elfadhil.
    Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi nne, Mwadui FC na Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex, Mtibwa Sugar na Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro, Simba SC na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Coastal Union na Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela dk78, Amksi tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk61.
    JKT Ruvu; Tony Kavishe, Michael Aidan, Napho Zuberi, Martin Kazila, Ramadhani Madenge, George Minja, Ismail Aziz/Abdulrahman Mussa dk57, Nashon Naftali, Samule Kamuntu/Gaudence Mwaikimba dk57, Saad Kipanga/Emmanuel Pius dk77 na Mussa Juma. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAZIDI KUTIMUA VUMBO LIGI KUU, YAITANDIKA JKT 4-1, SALAMU ZAO MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top