// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WATUA MORO KUVUNJA MWIKO MWINGINE, NI WA KUYANYASWA NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA JAMHURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WATUA MORO KUVUNJA MWIKO MWINGINE, NI WA KUYANYASWA NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA JAMHURI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Monday, September 28, 2015

        YANGA SC WATUA MORO KUVUNJA MWIKO MWINGINE, NI WA KUYANYASWA NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA JAMHURI

        MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA
        Septemba 30, 2015
        African Sports Vs Mgambo 
        Azam FC Vs Coastal Union
        Kagera Sugar Vs JKT Ruvu
        Mtibwa Sugar Vs Yanga SC
        Majimaji FC Vs Ndanda FC
        Prisons Vs Mwadui Fc
        Simba SC Vs Stand United
        Oktoba 1, 2015
        Toto Africans Vs Mbeya City
        Kikosi cha Yanga SC kilichoifunga Simba SC 2-0 Jumamosi Uwanja wa Taifa

        Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
        KIKOSI cha Yanga SC tayari kipo Morogoro tangu asubuhi kwa ajili yake mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar Jumatano.
        Yanga SC ambayo Jumamosi iliwazima watani, Simba SC kwa mabao 2-0 ya Amissi Tambwe na Malimi Busungu, imetua Morogoro na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo.
        Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu watafanya mazoezi Uwanja wa TANESCO leo jioni wakati kesho watafanya Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa mujibu wa kanuni ya mgeni kuutumia Uwanja wa mechi siku moja kabla.
        Kocha Mhoalanzi wa Yanga SC, Hans van der Pluijm atakuwa peke yake kwa maandalizi ya mchezo huo, kutokana na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa kwenda Iringa kwenye msiba wa mama mkwe wake.
        Na Yanga SC itamkosa beki wake Mkongo, Mbuyu Twite anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Simba SC Jumamosi. 
        Mtibwa Sugar wenye maskani yao, Turiani Morogoro wanatarajiwa kuingia Morogoro mjini mapema kesho kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
        Ikumbukwe, Yanga SC na Mtibwa wote wameshinda mechi zao nne za awali na Jumatano kila timu itawania ushindi mwingine ili kumondoa mpinzani kwenye mbio za ubingwa. 
        Na baada ya Yanga SC kufuta uteja kwa Simba SC Jumamosi, sasa inataka kuvunja mwiko wa kufungwa na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri keshokutwa.
        Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayoonyeshwa moja kwa moja kwa na Azam TV, inatarajiwa kuendelea Jumatano, African Sports itamenyana na ndugu zao, Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Azam FC na Coastal Union Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na Kagera Sugar na JKT Ruvu Uwanja wa A. H. Mwinyi Tabora.
        Mechi nyingine ni kati ya Mtibwa Sugar na Yanga SC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Majimaji FC na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji, Songea, Prisons na Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Simba SC na Stand United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Alhamisi Toto Africans itaikaribisha Mbeya City Uwanja CCM Kirumba, Mwanza.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: YANGA SC WATUA MORO KUVUNJA MWIKO MWINGINE, NI WA KUYANYASWA NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry