// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WALEEEE, PRISONS AFA 3-0 TAIFA…MSUVA LEO ALIKUWA MPISHI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WALEEEE, PRISONS AFA 3-0 TAIFA…MSUVA LEO ALIKUWA MPISHI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, September 16, 2015

    YANGA SC WALEEEE, PRISONS AFA 3-0 TAIFA…MSUVA LEO ALIKUWA MPISHI TU

    Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imeendelea kung’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 3-0 Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
    Mabingwa hao watetezi, sasa wanafikisha pointi sita na mabao matano, baada ya awali kushinda pia nyumbani 2-0 dhidi ya Coastal Union.
    Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Mkongo, Mbuyu Twite dakika ya 27 baada ya kipa wa Prisons, Mohammed Yussuf kushindwa kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na Simon Msuva, kufuatia Deus Kaseke kuangushwa nje ya boksi.
    Wachezaji wa Yanga SC wakimpongeza Mbuyu Twite baada ya kufunga bao la kwanza leo Uwanja wa Taifa

    Mrundi Amissi Tambwe aliifungia Yanga SC bao la pili dakika 45 akiumalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa Prison, Yussuf baada ya mpira wa adhabu wa kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima kufuatia Msuva tena kuangushwa.
    Mshambiliaji wa Prisons Jeremiah Juma alipoteza nafasi nzuri ya kufunga kipindi cha kwanza baada ya kupia juu la lango. Kipindi cha pili, kocha wa Prisons, Salum Mayanga alianza kwa kumpumzisha kipa Yussuf na kumuingiza Aron Kalambo
    Refa Alex Mahagi wa Mwanza alimtoa kwa kadi nyekundu James Josephat dakika ya 59 baada ya kumdondosha Msuva kwenye boksi na Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la tatu kwa penalti dakika ya 60.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa: Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Haji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke/Salum Telela dk66
    Simon Msuva, Haruna Niyonzima Geoffrey Mwashiuya dk79, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk84, Donald Ngoma na Deus Kaseke. 
    Prisons: Mohammed Yussuf/ Aron Kalambo dk46, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, James Josephat, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sabianka, Juma Seif, Mohammed Mkopi/Cosmas Ader dk47, Boniface Hau Ally Manzi dk64 na Jeremiah Juma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WALEEEE, PRISONS AFA 3-0 TAIFA…MSUVA LEO ALIKUWA MPISHI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top