// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC MABOSI LIGI KUU, WAITANDIKA COASTAL UNION 2-0 NA KUPANDA KILELENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC MABOSI LIGI KUU, WAITANDIKA COASTAL UNION 2-0 NA KUPANDA KILELENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 13, 2015

    YANGA SC MABOSI LIGI KUU, WAITANDIKA COASTAL UNION 2-0 NA KUPANDA KILELENI

    Mshambuliaji Donald Ngoma akipongezwa na Mzimbabwe mwenzake, Thabani Kamusoko baada ya kufunga bao la pili, Yanga SC ikiichapa 2-0 Coastal Union
    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Matokeo hayo yanaipeleka Yanga SC kileleni mwa LIgi Kuu baada ya mechi nane za mzunguko wa kwanza, ikiongoza kwa wastani wa mabao.
    Mchezaji bora na mfungaji bora wa LigiKuu msimu uliopita, Simon Happygod Msuva ndiye aliyefunga bao la kwanza la Yanga SC msimu huu, dakika ya saba akimalizia pasi ya Amisi Tambwe.
    Simon Msuva (kushoto) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
    Beki wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali (kushoto) akiwatoka wachezaji wa Coastal Union
    Beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi akiondosha mpira miguuni mwa winga wa Yanga SC, Godfrey Mwashiuya
    Mshambuliaji wa Yanga SC, Donald Ngoma akiwania mpira dhidi ya beki wa Coastal, Yassin Mustafa 

    Lilikuwa bao ambalo lilitokana na kazi nzuri ya yeye mwenyewe Msuva, aliyepokea pasi ya Haruna Niyonzima nje ya boksi na kuingia nayo ndani kabla ya kumpasia Tambwe aliyemrudishia mfungaji haraka kwa mbele kidogo.
    Kocha Mganda, Jackson Mayanja alifanya mabadiliko mapema tu baada ya bao hilo akimtoa mchezaji wa zamani wa Simba SC, Adeyoum Saleh Ahmed na kumuingiza mchezaji mwingine wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Twaha Ibrahim ‘Messi’.
    Mzimbabwe Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 42 na ushei akimalzia mpira uliodondoka baada ya kugongwa kwa kichwa na beki wa Coastal, Tumba Lui Swedi aliyeruka na Mrundi Amisi Tambwe kugombea krosi ya Simon Msuva.
    Kipindi cha pili, Coastal Union walibadilika na kucheza vizuri, lakini wakaishia kupoteza nafasi nzuri mbili kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa SImba SC, Ally Ahmed ‘Shiboli’.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela dk90, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk69, Donald Ngoma na Godfrey Mwashiuya/Deus Kaseke dk73.
    Coastal Union; Sabwato Nicholas Godfrey Wambura/Mbwana Hamisi ‘Kibacha’ dk62, Hamad Juma, Yassin Mustafa, Ernest Joseph Mwalupani, Tumba Swedi, Said Jeilan/Patrick Protas dk52, Ali Ahmad, Youssoufa Sabo, Nassor Kapama na Adeyoum Saleh Ahmed/Twaha Ibrahim ‘Messi’ dk22.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC MABOSI LIGI KUU, WAITANDIKA COASTAL UNION 2-0 NA KUPANDA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top