// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAKALI WA MUZIKI WA DANSI KUTAMBULISHA WIMBO “AMANI KWANZA” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAKALI WA MUZIKI WA DANSI KUTAMBULISHA WIMBO “AMANI KWANZA” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 14, 2015

    WAKALI WA MUZIKI WA DANSI KUTAMBULISHA WIMBO “AMANI KWANZA”

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    Wimbo maalum wa kuhimiza amani kabla na baada ya uchaguzi mkuu, utawekwa rasmi hadharani mbele ya waandishi wa habari Jumanne hii.
    Wimbo huo uliopewa jina la “Amani Kwanza” utapigwa ‘live’ kwa mara ya kwanza mbele ya wana habari ndani ya ukumbi wa nyuma wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam kuanzia saa 6 mchana.
    “Amani Kwanza” ni ngoma iliyopigwa katika miondoko ya rumba ikiwa imeshirikisha nyota wengi wa muziki wa dansi chini ya umoja  wa muda wa wanamuziki wa dansi na taarab.
    Mmoja wa magwiji wa muziki wa dansi nchini walioshiriki wimbo huo, King Kiki

    Mgeni rasmi katika tukio hilo anatarijiwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni bwana Paul Makonda.
    Mratibu wa ‘project’ hiyo Juma Mbizo alisema umoja huo haufungamani na dini, kabila wala chama chochote na kwamba lengo la ni moja tu – kusumbaza ‘mahubiri’ ya amani, umoja na mshikamano kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu.
    Mbizo amefafanua kuwa wimbo huo umerekodiwa katika studio za Sound Crafters chini ya producer Enrico huku video ikiwa imefanywa na King Dodoo.
    Wanamuziki waliotengeneza wimbo huo wako chini ya kamati inayoongozwa na Kanku Kelly ambaye ni mwenyekiti, katibu Omar Teggo, wajumbe ni Mafumu Bilal, King Dodoo na King Kiki huku Juma Mbizo akiwa mjumbe na mratibu.
    Mbizo amesema baada ya utambulisho huo, kila mwanahabari atapatiwa CD na DVD moja ya wimbo huo.
    “Lengo letu ni kutaka wanahabari wawatambue wasanii wote walioshiriki kutengeneza wimbo huo ikiwa ni pamoja na kuusikiliza ‘live’ hivyo naomba waandishi wa habari na wadau wa muziki waje kwa vingi Mango Garden Jumanne mchana,” alisema Juma Mbizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAKALI WA MUZIKI WA DANSI KUTAMBULISHA WIMBO “AMANI KWANZA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top