Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema klabu yake, TP Mazembe ya DRC inakabiliwa na mtihani mgumu katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani wapinzani wao El Merreikh ya Sudan ni wazuri.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwa simu kutoka Lubumbashi, Ulimwengu amesema pamoja na ukweli huo, lakini wamepania kuwang’oa.
“Merreikh ni wazuri, hilo hata sisi tunalijua, lakini tutawatoa tu,”amesema Uli na alipoulizwa watawezaje iwapo walishindwa kufurukuta kwa timu nyingine ya Sudan, El Hilal akasema; “Ile ilikuwa hatua ya makundi, sasa ni mtoano,”.
Ulimwengu amesema wanafahamu ubora wa timu za Sudan hususan Merreikh na mbinu zao zote za ndani na nje ya Uwanja, lakini wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanawatoa.
TP Mazembe itamenyana na El Merreikh katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa kwanza ukichezwa Septemba 25, mwaka huu mjini Khartoum na marudiano Oktoba 2 mjini Lubumbashi.
Huo ni mtihani mkubwa kwa Mazembe, kwani imekuwa ikisumbuliwa mno na timu za Sudan- katika hatua ya makundi mwaka huu ilipangwa na El Hilal na haikushinda hata mchezo mmoja.
Mchezo wa kwanza Lubumbashi ililazimishwa sare kabla ya kufungwa 1-0 mchezo wa marudiano Sudan- na saa wanakutana na timu ambayo inaaminika ndiyo bora zaidi nchini humo.
Nusu Fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa kati ya El Hilal ya Sudan na USM Alger ya Algeria, nao pia mechi ya kwanza itakuwa Septemba 25 na marudiano Oktoba 2, mwaka huu.

Thomas Ulimwengu amekiri Merreikh ni wazuri, lakini amesema TP Mazembe itawatoa |

0 comments:
Post a Comment