// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UHOLANZI 'MAJI YA SHINGO' KUFUZU EURO 2016, YAPIGWA KIDUDE NWA ICELAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UHOLANZI 'MAJI YA SHINGO' KUFUZU EURO 2016, YAPIGWA KIDUDE NWA ICELAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 04, 2015

    UHOLANZI 'MAJI YA SHINGO' KUFUZU EURO 2016, YAPIGWA KIDUDE NWA ICELAND

    Nahodha mpya wa Uholanzi, Arjen Robben alitoka uwanjani baada ya dakika 27 tu kufuatia kuumia nyonga PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    TIMU ya taifa ya soka ya Iceland imejisogeza kukata tiketi ya kufuzu kucheza mchuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016 baada ya ushindi wa penalti ya utata ya Gylfi Sigurdsson w 1-0 dhidi ya Uholanzi waliomaliza pungufu ya mchezaji mmoja usiku wa jana.
    Refa Milorad Mazic wa Serbia, aliyemtoa kwa kadi nyekundu Martins Indi dakika ya 33, aliwazawadia mkwaju wa penalti Iceland dakika ya  51 ingawa Gregory van der Wiel alionekana kuuwahi moira wakati anapambana na Birkir Bjarnason. 
    Sigurdsson akaenda kufunga penalti hiyo akimtungua kipa Jasper Cillessen na kuiweka Iceland katika mazingira mazuri ya kukata tiketi ya kwanza ya fainali za michuano mikubwa. 
    Matokeo hayo yanaiweka Uholanzi katika mazingira magumu kidogo katika kundi hilo A kutokana na Iceland kutimiza pointi 18, mbili zaidi ya Jamhuri ya Czech wanaoshika nafasi ya pili. Uholanzi inabaki na pointi zake 10.
    Iceland sasa wanaweza kujihakikishia kucheza Euro 2016 iwapo tu watashinda mchezo wa nyumbani dhidi ya Kazakhstan Jumapili.
    Kipigo hicho kinamuweka pabaya kocha mpya wa Uholanzi, Danny Blind. Kocha aliyetangulia Guus Hiddink alilazimika kujiuzulu kwa sababu ya matokro mabaya hususan baada ya timu hiyo kufungwa mabao 2-0 nchini Iceland mwezi Oktoba.
    Mshambuliaji Robin van Persie, ambaye aliiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil zaidi ya mwaka mmoja uliopita, jana aliwekwa benchi na kocha Blind. 

    MECHI ZILIZOSALIA

    Septemba 6; 
    Latvia vs Jamhuri ya Czech Uturuki vs Uholanzi
    Iceland vs Kazakhstan
    Oktoba 10 
    Iceland vs Latvia, Kazakhstan vs Uholanzi Jamhuri ya Czech vs Uturuki
    Oktoba 13
    Latvia vs Kazakhstan; Uholanzi vs Jamhuri ya Czech 
    Uturuki vs Iceland
    Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Van der Wiel, De Vrij, Martins Indi, Blind, Wijnaldum/Promes dk80, Klaassen, Robben/Narsingh dk31, Sneijder, Depay na Huntelaar/Bruma dk40.
    Iceland; Halldorsson, Saevarsson, Arnason, Ragnar Sigurdsson, Ari Freyr Skulason, Bodvarsson/Finnbogason dk78, Gylfi Sigurdsson, Gunnarsson/Olafur Ingi Skulason dk86,Birkir Bjarnason, Gudmundsson na Sigthorsson/Gudjohnsen dk64).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UHOLANZI 'MAJI YA SHINGO' KUFUZU EURO 2016, YAPIGWA KIDUDE NWA ICELAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top