// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TWIGA STARS ‘YAWAAGA VIZURI’ WAKONGO MICHEZO YA AFRIKA, YAMALIZA NAFASI YA TATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TWIGA STARS ‘YAWAAGA VIZURI’ WAKONGO MICHEZO YA AFRIKA, YAMALIZA NAFASI YA TATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 13, 2015

    TWIGA STARS ‘YAWAAGA VIZURI’ WAKONGO MICHEZO YA AFRIKA, YAMALIZA NAFASI YA TATU

    TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi A Michezo wa Afrika mbele ya wenyeji Kongo Brazzaville.
    Hiyo inafutaia Twiga Stars kulazimisha sare ya 1-1 na wenyeji Kongo jana mjini Kintele katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A.
    Dedina Mbondzo alianza kuifungia Kongo kipindi cha kwanza, kabla ya Shelder Boniface Mafuru kuisawazishia Twiga Stars dakika ya 52.

    Zote Tanzania na Kongo zimemaliza na pointi moja, baada ya kupoteza mechi zao mbili za awali dhidi ya Nigeria na Ivory Coast, lakini wenyeji wamefungwa mabao mengi ndiyo maana wanashika mkia.  
    Ivory Coast imemaliza kileleni mwa kundi hilo kwa kukusanya jumla ya pointi tisa, baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Nigeria mabao 2-1 jana. Nigeria imemaliza na pointi sita.
    Kwa upande wa wanaume, mabingwa watetezi Ghana wametolewa baada ya Senegal kulazimishwa sare ya 1-1 na Nigeria katika mchezo wa Kundi B jana Uwanja wa Unity mjini Kintele.
    Nigeria imeongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, ikifuatiwa Senegal pointi mbili huku Ghana ikimaliza na pointi moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS ‘YAWAAGA VIZURI’ WAKONGO MICHEZO YA AFRIKA, YAMALIZA NAFASI YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top