// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TP MAZEMBE KUIVAA EL MERREIKH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, KATUMBI ASEMA; “SAMATTA NI MCHEZAJI BABU KUBWA” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TP MAZEMBE KUIVAA EL MERREIKH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, KATUMBI ASEMA; “SAMATTA NI MCHEZAJI BABU KUBWA” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, September 15, 2015

    TP MAZEMBE KUIVAA EL MERREIKH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, KATUMBI ASEMA; “SAMATTA NI MCHEZAJI BABU KUBWA”

    NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA:
    Septemba 25, 2015
    El Merreikh Vs TP Mazembe
    El Hilal Vs USM Alger
    Oktoba 2, 2015
    TP Mazembe Vs El Merreikh
    USM Alger Vs El Hilal
    Mbwana Samatta alifunga mabao matatu peke yake Mazembe ikishinda 5-0 mwishoni mwa wiki

    TP Mazembe itamenyana na El Merreikh ya Sudan katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa kwanza ukichezwa Septemba 25, mwaka huu mjini Khartoum na marudiano Oktoba 2 mjini Lubumbashi.
    Huo ni mtihani mkubwa kwa Mazembe, kwani imekuwa ikisumbuliwa mno na timu za Sudan- katika hatua ya makundi mwaka huu ilipangwa na El Hilal na haikushinda hata mchezo mmoja.
    Mchezo wa kwanza Lubumbashi ililazimishwa sare kabla ya kufungwa 1-0 mchezo wa marudiano Sudan- na saa wanakutana na timu ambayo inaaminika ndiyo bora zaidi nchini humo. 
    Nusu Fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa kati ya El Hilal ya Sudan na USM Alger ya Algeria, nao pia mechi ya kwanza itakuwa Septemba 25 na marudiano Oktoba 2, mwaka huu.
    Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe amefurahia ushindi wa 5-0 katika mchezo wa mwisho mwishoni mwa wiki dhidi ya Moghreb Tetouan YA Morocco na kuongoza Kundi A, Mbwana Ally Samatta wa Tanzania akifunga mabao matatu.
    “Kabla ya mchezo, nilitarajia mabao mawili kwa Mbwana Samatta. Ni mchezaji babu kubwa ambaye aliibuka baada ya kipindi kigumu alichopitia. Wakati wote nawaamini wachezaji, kwa sababu kuna wakati wanakuwa hawajisikii vizuri. Mbwana Samatta amefunga, tunatarajia kufanya vizuri zaidi,”amesema katumbi.
    Ikumbukwe, safari ya Merreikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilianzia Dar es Salaam ambako ilifungwa 2-0 na Azam FC, kabla ya kwenda kushinda 3-0 nyumbani katika mchezo wa marudiano na kusonga mbele.
    Bilionea Moise Katumbi Chapwe amesema Mbwana Samatta ni mchezaji babu kubwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TP MAZEMBE KUIVAA EL MERREIKH NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, KATUMBI ASEMA; “SAMATTA NI MCHEZAJI BABU KUBWA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top