// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TOM SAINTFIET AENDELEA KUING'ARISHA TOGO, YASHINDA 2-0 KUFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TOM SAINTFIET AENDELEA KUING'ARISHA TOGO, YASHINDA 2-0 KUFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 05, 2015

    TOM SAINTFIET AENDELEA KUING'ARISHA TOGO, YASHINDA 2-0 KUFUZU AFCON

    KOCHA wa zamani wa Yanga SC, Mbelgimji Tom Saintfiet ameiwezesha Togo kushinda mechi ya pili mfululizo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika baada ya jana kuifunga 2-0 Djibouti.
    Togo ambayo ilimkosa nyota wake, Emmanuel Adebayor aliyekataa kujiunga na timu baada ya kupokonywa Unahodha katika mchezo uliopita wakishinda 2-1 dhidi ya Liberia mweziu June.
    Nahodha mpya, Serge Akakpo aliifungia  bao la kwanza Togo dakika ya tatu kabla ya Jonathan Ayite kufunga la pili kipindi chakwanza na sasa Togo inaongoza Kundi A kwa pointi zake sita.
    Mechi nyingine ya kundi hilo leo Tunisia watamenyana na Liberia. Huo utakuwa mchezo wa kwanza kuchezwa mjini Monrovia tangu ufungiwe kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola.
    Tunisia iliifunga 8-1 Djibouti katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo Juni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOM SAINTFIET AENDELEA KUING'ARISHA TOGO, YASHINDA 2-0 KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top