// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TANZANIA YABORONGA 'HAKUNA MFANO' MICHEZO YA AFRIKA KONGO-BRAZAVILLE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TANZANIA YABORONGA 'HAKUNA MFANO' MICHEZO YA AFRIKA KONGO-BRAZAVILLE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, September 17, 2015

    TANZANIA YABORONGA 'HAKUNA MFANO' MICHEZO YA AFRIKA KONGO-BRAZAVILLE

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    WANAMICHEZO wa hapa nchini waliokuwa wanachuana katika Michezo ya Afrika mwaka huu (All Africa Games 2015) wametoka mikono mitupu baada ya kufanya vibaya katika michezo mbalimbali waliyoshiriki katika fainali hizo zinazotarajiwa kumalizika kesho Jumamosi huko Kongo Brazaville.
    Timu ya Tanzania iliwakilishwa katika michezo ya ngumi, riadha, judo, kuogelea, Paralimpiki (walemavu) na soka la wanawake.

    Wachezaji wa timu ya Tanzania wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania wakati wanakwenda Kongo Brazaville kwenye Michezo ya Afrika. Timu hiyo imerejea mikono mitupu

    Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya,  alisema kwa njia ya simu jana kuwa wanariadha ambao walibakia wakipeperusha bendera ya nchi jana nao walishindwa kung'ara na kuifanya timu ya Tanzania kukosa medali ya aina yoyote.
    "Tumeshindwa kupata medali hata moja, tunasikitika hata katika mchezo wa riadha ambao tumekimbia jana (juzi) pia tumeshindwa," alisema Lihaya.
    Alisema kati ya wanariadha wanne waliokimbia jana,Ally Khamis Gulam, ambaye aliingia hatua ya nusu fainali katika mita 200 naye hakufanya vizuri kwa kushindwa kupata nafasi ya kufika hatua ya fainali.
    Alisema kwamba changamoto kubwa waliyojifunza ni timu kutoka nchi nyingine kufanya maandalizi ya muda mrefu tofauti na wanamichezo wa Tanzania na uchache wa washiriki waliokwenda kushiriki michezo hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YABORONGA 'HAKUNA MFANO' MICHEZO YA AFRIKA KONGO-BRAZAVILLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top