// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YAKAMILIKA TAYARI KUMUANGAMIZA 'TAI MKUBWA' JUMAMOSI DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YAKAMILIKA TAYARI KUMUANGAMIZA 'TAI MKUBWA' JUMAMOSI DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, September 03, 2015

    TAIFA STARS YAKAMILIKA TAYARI KUMUANGAMIZA 'TAI MKUBWA' JUMAMOSI DAR

    WACHEZAJI watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.
    Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.
    Mshambuliaji tegemeo wa Taifa Stars, Mbwana Samatta tayarinyupo kambini kwa ajiliya mechi na Nigeria Jumamosi

    Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
    Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
    Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAKAMILIKA TAYARI KUMUANGAMIZA 'TAI MKUBWA' JUMAMOSI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top