Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imefanikiwa kupata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya beki wake wa pande zote mbili za pembeni, Emery Nimubona- maana yake atacheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC inaanzia Uwanja wa Mkwakani, Tanga kesho dhidi ya wenyeji African Sports na hadi jana ilikuwa haijapata ITC ya Nimubona iliyemsajili kutoka Vital’O ya Burundi.
Lakini jioni hii, Kaimu Kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collin Frisch ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE kwamba baada ya kupatikana kwa ITC ya Nimubona, sasa wachezaji wote saba wa kigeni wako huru kucheza Ligi Kuu.
Wachezaji wengine wapya wa kigeni wa Simba SC ni kipa Vincent Angban wa Ivory Coast, kiungo Justuce Majabvi wa Zimbabwe na washambuliaji Hamisi Kiiza wa Uganda, Pape Abdoulaye N'Daw wa Senegal ambao wote ITC zao zimefika.
Watano hao wanaungana na Waganda wawili, beki Juuko Murushid na mshambuliaji Simon Sserunkuma kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu.
Maana yake kikosi cha Simba SC kipo kamili kuelekea mchezo wa kesho wa ufunguzi wa Ligi Kuu Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya Wana Kimanumanu.

Emery Nimubona amepata ITC na atacheza kesho dhidi ya Sports Mkwakwani |
Wachezaji wengine wapya wa kigeni wa Simba SC ni kipa Vincent Angban wa Ivory Coast, kiungo Justuce Majabvi wa Zimbabwe na washambuliaji Hamisi Kiiza wa Uganda, Pape Abdoulaye N'Daw wa Senegal ambao wote ITC zao zimefika.
Watano hao wanaungana na Waganda wawili, beki Juuko Murushid na mshambuliaji Simon Sserunkuma kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu.
Maana yake kikosi cha Simba SC kipo kamili kuelekea mchezo wa kesho wa ufunguzi wa Ligi Kuu Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dhidi ya Wana Kimanumanu.
0 comments:
Post a Comment