Na Princess Asia, TANGA
SIMBA SC imetimiza dhamira ya kukusanya pointi zote sita katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara- baada ya jioni ya leo kuilaza mabao 2-0 JKT Mgambo.
Huo ni mwanzo mzuri kwa kocha Muingereza Dylan Kerr Simba SC, kwani sasa Wekundu wa Msimbazi nao wamo kwenye mbio za ubingwa.
Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Mzimbabwe Justuce Majabvi dakika ya 27 baada ya krosi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuzua kizazaa langoni mwa Mgambo.
Mgambo walikosa bao la wazi dakika ya 19 baada ya shuti la Salim Aziz Gillah kupaa juu kidogo ya lango.
Said Ndemla alikaribia kufunga dakika ya 35 kwa kichwa akimaizia krosi ya Hassan Kessy lakini mpira ukatoka nje kidogo ya lango.
Mgambo tena wakakosa bao la wazi baada ya shuti la Nassor Gumbo aliyeingia akichukua nafasi ya Salim Gillah kugonga mwamba na kurudi uwanjani dakika tano baaadye.
Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 73 akimalizia pasi Ibrahim Hajibu baada ya gonga safi baina yao.
Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba SC baada ya awali kuifunga African Sports 1-0, bao pekee la Kiiza.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, Mohamed Hussein, Hassan Ramadhani, Murushid Juuko, Hassan Isihaka, Justuce Majabvi, Awadh Juma, Said Ndemla/Abdoulaye Pape N’daw dk69, Mussa Mgosi/Ibrahim Habib dk67, Mwinyi Kazimoto/Hamisi Kiiza dk46 na Peter Mwalianzi.
Mgambo JKT; Said Abdi, Bashiru Chanache, Salim Mlima, Salim Kipaga, Ramadhani Malima/Athanas Chacha, Bakari Mtama, Salim Gillah, Mohammed Samatta, Helbert Charles, Fullu Zulu Maganga/Bolly Shaibu dk68 na Chande Magoja.

Wachezaji wa Simba SC wakimpongeza Justuce Majabvi kushoto baada ya kufunga bao la kwanza |

0 comments:
Post a Comment