// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC IMEONEA ‘VIDIGIDIGI’, ASEMA KOCHA AFRICAN SPORTS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC IMEONEA ‘VIDIGIDIGI’, ASEMA KOCHA AFRICAN SPORTS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 13, 2015

    SIMBA SC IMEONEA ‘VIDIGIDIGI’, ASEMA KOCHA AFRICAN SPORTS

    Na Princess Asia, TANGA
    KOCHA Mkuu wa African Sports ya Tanga, Joseph Lazaro amesema kwamba uzoefu mdogo wa wachezaji wake, ndiyo uliigharimu timu hiyo kulala 1-0 mbele ya Simba SC katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Mkwakwani.
    Lazaro alisema kuwa Simba ilifanikiwa kushinda mchezo huo kutokana na uzoefu wa wachezaji wake ukilinganisha na nyota wake ambao wengi wametoka kwenye timu yao ya vijana.
    "Tumefungwa kwa sababu ya jambo moja, uzoefu na si jingine, suala la uzoefu limesimama pale pale, Simba walikuwa wakitaka kutulia wanatulia," alisema Lazaro.
    Aliongeza kuwa timu yake itaimarika na kadri watakavyocheza mechi zaidi na wasitarajie kuwakuta vile vile kwenye mechi ya marudiano.
    Kikosi cha African Sports kilichofungwa 1-0 na Simba SC jana
    Kocha Lazaro (kushoto) akiwa na Msaidizi wake, Rzack Ssiwa kulia



    " Uwezo wetu wa kucheza utaongezeka, hofu pia ilichangia kuwasumbua wscgezaji wangu, hawakufuata kile nilichokuwa nawakumbusha, ila kiufundi wako vizuri," alisema beki huyo wa zamani wa Yanga SC.
    Alisema pia wachezaji wake hawakuwa na bahati ya kufunga kwa kupoteza nafasi mbili za wazi katika dakika za lala salama za mchezo huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC IMEONEA ‘VIDIGIDIGI’, ASEMA KOCHA AFRICAN SPORTS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top