// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA APIGA HAT TRICK MAZEMBE YAUA 5-0 LIGI YA MABINGWA, YATINGA NUSU FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA APIGA HAT TRICK MAZEMBE YAUA 5-0 LIGI YA MABINGWA, YATINGA NUSU FAINALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 12, 2015

    SAMATTA APIGA HAT TRICK MAZEMBE YAUA 5-0 LIGI YA MABINGWA, YATINGA NUSU FAINALI

    MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata mabao matatu jioni ya leo TP Mazembe ikishinda 5-0 dhidi ya Moghreb Tetouan ya Morocco Uwanja wa Mazembe, Lubumbashi, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Na kwa matokeo hayo, Mazembe inakwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kufikisha pointi 11 na kupanda kileleni mwa Kundi A, mbele ya El Hilal ya Sudan yenye pointi tisa, Moghreb pointi nane na Smouha ya Misri pointi nne.
    Samatta alifunga mabao hayo dakika ya 12, 53 na 90 na akatoa pia pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Rainford Kalaba dakika ya 12, huku bao lingine likifungwa na Rogger Assale dakika ya 88.
    Mshambuliaji mwingine wa Tanzania, Thomas Ulimwengu alikuwa benchi muda wote wa mchezo wa leo kutokana na maumivu aliyoyapata akiicheza Taifa Stars dhidi ya Nigeria. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA APIGA HAT TRICK MAZEMBE YAUA 5-0 LIGI YA MABINGWA, YATINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top