// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PIGO LINGINE SUPER EAGLES KUELEKEA MECHI NA STARS, BEKI MRITHI WA JOSEPH YOBO NAYE ‘HOI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PIGO LINGINE SUPER EAGLES KUELEKEA MECHI NA STARS, BEKI MRITHI WA JOSEPH YOBO NAYE ‘HOI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 04, 2015

    PIGO LINGINE SUPER EAGLES KUELEKEA MECHI NA STARS, BEKI MRITHI WA JOSEPH YOBO NAYE ‘HOI’

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    BEKI Leon Balogun anayechezea FSV Mainz ya Ujerumani leo ameshindwa kufanya mazoezi na timu yake ya taifa, Nigeria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na maumivu ya nyama.
    Lakini kocha wa Super Eagles, Sunday Oliseh amesema hana wasiwasi atapata matokeo mazuri kesho mbele ya wenyeji Tanzania, Taifa Stars katika mchezo huo wa Kundi G kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.
    Kikosi cha Super Eagles jioni ya leo kimefanya mazoezi mepesi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tangu wawasili jana usiku kuelekea mchezo huo wa kesho.
    Leon Balogun hakufanya mazoezi na Nigeria leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na maumivu ya nyama 

    Kocha wa Nigeria, Sunday Oliseh akijiandaa kwa kazi Uwanja wa Taifa leo

    Na Balogun mzaliwa wa baba Mnigeria na mama Mjerumani, aliyeitwa kwa mara ya kwanza Super Eagles Machi mwaka jana kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mexico kuchukua nafasi ya Joseph Yobo alikuwa benchi leo wakati wenzake wanafanya mazoezi.
    “Anasumbuliwa na maumivu ya nyama kidogo, nimeamua kumpumzisha,”alisema Oliseh akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo.
    Kiungo huyo wa zamani wa Nigeria amesema kwamba Tanzania si timu ya kubeza japokuwa haina jina kubwa na wataingia katika mchezo wa kesho kucheza kwa bidii kusaka matokeo mazuri.
    “Hatuwezi kuwadharau wenyeji wetu, kweli hawana wachezaji wanaocheza Ulaya, lakini nimewaangalia ni timu nzuri na tunatarajia ushindani kesho,”amesema. 
    Oliseh amemchukua kipa wa Enyimba ya nyumbani, Nigeria Femi Thomas kuziba pengo la Nahodha, Vincent Enyeama ambaye amejitoa kikosini kwa matatizo ya kifamilia.
    Femi alikuwa pamoja na Carl ikeme wa Wolves ya England na Ezenwa Ikechukwu wa Sunshine Stars ya Nigeria wakifanya mazoezi leo- mmojawao ndiye ataanza kesho.
    Kocha Sunday Oliseh akitoa maelekezo kwa wachezaji wake leo Uwanja wa Taifa


    Wachezaji wa Super Eagles wakifanya mazoezi mepesi leo Uwanja wa Taifa

    Super Eagles wakiomba dua kabla ya kuanza mazoezi leo Uwanja wa Taifa

    Mabeki waliokuja na kikosi cha Eagles ni Thomas Olufemi, Leon Balogun, Kwambe Solomon, Omeruo Keneth, Ekong William, Oboroakpo Austin, Akasi Chima, na Madu Kingsley.
    Viungo ni Ibrahim Rabiu, Muhamed Usman, Uzochukwu Izunna, Haruna Lukman, Nwankwo Obiora, Igboun Emeka, wakati washambuliaji ni Simon Daddy, Ujah Anthony, Emenike Chinenye, Musa Ahmed, Aggreh Obus na Eduok Samuel.
    Mchezo huo unatarajiwa kuanza kesho Saa 10:30 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na utachezeshwa na marefa kutoka Rwanda, wanaotarajiwa kuwasili usiku wa leo.
    Nigeria wana pointi tatu baada ya ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Chad, wakati Tanzania inashika mkia ikiwa haina pointi baada ya kufungwa 3-0 na Misri katika mchezo wa kwanza ugenini. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Mafarao wa Misri watakuwa wageni wa Chad. 
    Kipa anayetarajiwa kuanza kesho, Carl Ikeme akidaka shuti mazoezini leo


    Kipa Femi Thomas aliyeitwa kuziba pengo la Vincent Enyeama akiruka juu kuokoa  

    Wachezaji wa Nigeria wakifanya mazoezi ya kuchangamsha misuli leo Uwanja wa Taifa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO LINGINE SUPER EAGLES KUELEKEA MECHI NA STARS, BEKI MRITHI WA JOSEPH YOBO NAYE ‘HOI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top