Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa mchango wa shilingi milioni 10, 486,000 kwa ajili ya mandalizi ya sherehe ya kumuaga Rais Jamhuri ya Mungano Dk Jakaya Kikwete ambaye atastaafu hivi karibuni inayoandaliwa na Wandishi wa habari nchini.
Mchango huu umetolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kupitia Chama cha Wandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA)
Meneja Uhusiano wa NCAA, Adam Akyoo amesema mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari Dar es Salaam kwamba, Mamlaka imetoa mchango huo kwa sababu Kikwete, ni mdau mkubwa wa Hifadhi ya Ngorongoro tangu alipokuwa Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Na amesema Kikwete ndiye Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania aliyetembelea hifadhi hii mara nyingi zaidi kuliko viongozi wengine wote wa Taifa waliomtangulia.
"Pia amekuwa mdau muhimu na wa mstari wa mbele wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika kutangaza vyema vivutio vya watalii vya hifadhi ya Ngorongoro katika mataifa mbali mbali duniani alikokwenda kwa ziara za kikazi,"amesema.
|
Mhando, Akyoo na Grace Hoka katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam |
0 comments:
Post a Comment