KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa leo ametoa pasi za mabao mawili, timu yake, Free State Stars ya Afrika Kusini ikipata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Absa baada ya kuifunga mabao 3-0 Chippa United.
Ngassa ambaye alichezeshwa nafasi ya kiungo leo, alitoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Andrea Fileccia dakika ya 34 na la tatu lililofungwa na Andrea Fileccia dakika ya 84.
Bao la tatu la FS katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa nyumbani, lilifungwa na Danny Venter dakika ya 77.
Huo ni mwanzo mzuri kwa kocha mpya Mjerumani Ernst Middendorp aliyerithi mikoba ya Mmalawi Kinnah Phiri aliyejiuzulu baada ya timu kupoteza mechi tatu mfululizo za mwanzo katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini 1-0 kutoka kwa Mpumalanga Blac Aces, 4-0 kutoka kwa Kazier Chiefs na 2-1 mbele ya Ajax Cape Town.
Ngassa alisajiliwa Mei mwaka huu na Free State ya Bethelehem baada ya kocha Phiri kuvutiwa na soka yake akiwa anacheza Yanga SC ya Tanzania, leo alikuwa kivutio mno akicheza nafasi ya kiungo.
Kikosi cha Free State Stars kilikuwa; Diakite, Masehe, Mashego, Shabalala, Sankara, Tlhone, Ngasa, Somaeb/Mothiba dk70, Fileccia/Thethani dk86, Obada/Mohomi dk45 na Venter.
Chippa United: Masiko, Okwuosa, Thopola/Zuke dk47, Macheka, Chipeta, Sali, Molangoane, Mthiyane/Twala dk52, Mayambela, R. Manzini/L. Manzini dk55 na Cloete.

Nyota ya Mrisho Ngassa imeanza kung'ara Afrika Kusini |

0 comments:
Post a Comment