MWIMBAJI nguli wa muziki wa dansi Mwinjuma Muumin ameipa pigo kubwa Twanga Pepeta baada ya kuwanyakua waimbaji tegemeo wa bendi hiyo Saleh Kupaza na Dogo Rama. Hivi unavyosoma habari hii, tayari wanamuziki hao wako nchini Msumbiji na wanatarajiwa kuwa huko kwa mwezi mzima.
Muumin na bendi yake ya Double M Sound amepata mwaliko wa mwezi mzima wa kufanya maonyesho katika miji mbali mbali ya Msumbiji. Kikosi cha wanamuziki 17 akiwemo Dogo Rama na Saleh Kupaza, kiliondoka Jumatatu asubuhi kuelekea Msumbiji.
Kwa mujibu wa Saluti5, Muumin amethibitisha Dogo Rama na Saleh Kupaza wameondoka na Double M Sound lakini alikataa kuthibitisha iwapo amewasajili jumla au amewachukua kwa mkopo.
“Wale ni swahiba zangu, hatushindwani kitu, tutafanya maongezi ya kina huko Msumbiji na kama tutaafikiana basi Kupaza na Dogo Rama watakuwa mali ya Double M Sound,” alisema Muumin.

Muumin Mwinjuma akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kwa safari ya Msumbiji |
Kwa mujibu wa Saluti5, Muumin amethibitisha Dogo Rama na Saleh Kupaza wameondoka na Double M Sound lakini alikataa kuthibitisha iwapo amewasajili jumla au amewachukua kwa mkopo.
“Wale ni swahiba zangu, hatushindwani kitu, tutafanya maongezi ya kina huko Msumbiji na kama tutaafikiana basi Kupaza na Dogo Rama watakuwa mali ya Double M Sound,” alisema Muumin.
0 comments:
Post a Comment