MTANZANIA Julio Ludago amedhamiria kuvunja rekodi ya dunia kwa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa muda mfupi zaidi.
Hadi sasa raia wa Uswisi, Ecuadorian Karl ndiye anashikilia rekodi hiyo aliyoiweka mwaka mwezi August, 2014 ambapo alitumia masaa 9 na dakika 16.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ludago alisema amefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha anatimiza azma yake hiyo.
Ludago ambaye amekuwa akifanya kazi za kuwaongoza watalii kwa muda mrefu alisema amekuwa akisikitishwa na kitendo cha wageni kuja na kufanikiwa kuvunja rekodi hiyo.
"Nimekuwa nikishuhudia wageni wakija na kuvunja rekodi hivyo nikaona nijifue ili nirudishe heshima ya Tanzania,"alisema
"Nimefanya mazoezi kwa muda mrefu na sasa niko tayari kupanda mlima Kilinanjaro na kuvunja rekodi,"aliongeza
Aidha, Ludago amewashukuru wadhamini mbalimbali ambao wamempa sapoti katika maandalizi yangu kwa namna moja ama nyingine.
Ludago (35) mwenye asili ya mkoa wa Iringa anatarajiwa kupanda mlima huo Septemba 17.
Naye mwakilishi wa kampuni ya Intel ambao ni wamekuwa wakimdhamini Ludago katika maandalizi yake, Radhia alisema wanaamini atavunja rekodi hiyo na kuiletea sifa nchi.
"Kupitia kampuni yetu tuliweza pia kumpatia vifaa mbalimbali katika maandalizi yake ya kupanda mlima mrefu zaidi Afrika, tunaamini atatimiza malengo yake,"alisema.

0 comments:
Post a Comment